LIVE:RAIS SAMIA AKIWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI ALIOWATEUA


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Viongozi wateule, Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 13 Septemba, 2021. Viongozi wanaoapishwa ni:


Mhe. Dkt. STERGOMENA LAWRENCE TAX (Mb), kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

2. Mhe. Dkt. ASHATU KACHWAMBA KIJAJI (Mb), kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

3. Mhe. JANUARY YUSUF MAKAMBA (Mb), kuwa Waziri wa Nishati.

4. Mhe. Prof. MAKAME MNYAA MBARAWA (Mb), kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.

5. Amemteua Dkt. ELIEZER MBUKI FELESHI, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

YALIYOJIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi kufanya kazi kwa vitendo zaidi badala ya kutoa maneno makali akisema Serikali itaendeshwa kwa matendo makali siyo maneno makali.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatatu Septemba 13,2021 wakati akiwaapisha Mawaziri Watatu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

"Kipindi cha miezi sita nilikuwa najifunza, Nilikuwa Makamu wa Rais, nilikuwa na nyinyi lakini sikuwa na fursa ya ndani ya kujifunza utendaji wa ndani ya Wizara mbalimbali. Nimekuwa nikijifunza na nimeona sasa vipi nakwenda na nyie.

Katika uongozi kuna mbinu nyingi. Nami nimejichagulia mbinu yangu. Nataka niwaambie kuwa tunakoendelea huko Serikali yetu itaendeshwa kwa matendo makali na siyo maneno makali. Ninaposema matendo makali wala siyo kupigana mijeledi, ni kwenda kwa wananchi kutoa huduma inayotakiwa, kila mtu kufanya wajibu wake,"amesema Rais Samia.

"Msinitegemee kwa maumbile yangu haya, pengine na malezi yangu kukaa hapa nianze kufoka weyee..wawawaaaaa! Nahisi siyo heshima, na kwa sababu nafanya kazi na watu wazima, wanaojua jema na baya ni lipi. 

"Kwa hiyo ni imani yangu kwamba tunapozungumza tunaelewana na kila mtu anajua afanye nini kwenye wajibu wake. Kwa hiyo msitegemee nianze kufoka ovyo ovyo, kufokea watu wazima wenzangu,"amesema Rais Samia.

Post a Comment

0 Comments