Mjumbe wa UWT, Rhobi Samwelly aazimia makubwa kuhusu elimu Mara

Na Fresha Kinasa, Diraakini Blog

Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake (UWT) Taifa Mkoa wa Mara, Rhobi Samwelly, amesema atashirikiana na jumuiya hiyo mkoani humo kuanzisha mfuko wa elimu kwa lengo la kuwawezesha watoto wa kike kusoma na kufikia malengo yao kusudi ije iwasaidie kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo yao na taifa kwa ujumla.
Mjumbe wa Baraza la UWT Taifa Mkoa wa Mara, Rhobi Samwelly akizungumza katika kikao cha Baraza la UWT Wilaya ya Serengeti. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Serengeti, Jacob Bega na viongozi mbalimbali wa jumuiya na chama hicho.

Rhobi ameyasema hayo leo Septemba 4, 2021 wakati akizungumza na Wajumbe wa Baraza la UWT Wilaya ya Serengeti mkoani Mara katika kikao cha baraza la kawaida kilichofanyika ukumbi wa CCM wilayani humo, ambapo pamoja na mambo mengine amesema jumuiya hiyo ina jukumu la kubuni miradi mbalimbali itakayoiingizia vipato jumuiya sambamba na kuongeza vipato vyao katika familia na hivyo kuwakwamua kiuchumi.

"Watoto wa kike wakisoma wana mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi katika jamii na taifa letu, naahidi kushirikiana na jumuiya kuanzisha mfuko wa elimu utakaotatua changamoto ambazo huwakwamisha watoto wa kike wasitimize ndoto zao. Nafahamu zipo baadhi ya mila kandamizi dhidi yao ambazo huwanyima fursa ya kufika mbali, lazima kwa pamoja tushiriki kuzipinga ikiwemo ukeketaji na ndoa za utotoni," amesema Rhobi.

Ameongeza kuwa, mfuko huo utaweza kutatua changamoto mbalimbali na kuwaendeleza katika fani mbalimbali za ufundi stadi na vyuo vinavyotoa fani zingine katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kutatua changamoto ya ajira na kuwawezasha kujiajiri na kuondokana na utegemezi.
Mjumbe wa Baraza la UWT Taifa Mkoa wa Mara, Rhobi Samwelly akikabidhi cheti kwa mmoja wa wadau ambao wamekuwa wakiisaidia jumuiya hiyo kutambua mchango wao.
Mjumbe wa Baraza la UWT Taifa Mkoa wa Mara, Rhobi Samwelly akikabidhi cheti kwa mmoja wa wadau ambao wamekuwa wakiisaidia Jumuiya hiyo kutambua mchango wao.
Katika hatua nyingine Rhobi amewahimiza Wajumbe wa Jumuiya hiyo, kusimama kidete kupigania maendeleo na uhai wa jumuiya hususani kwa kuhakikisha wanachama wa jumuiya hiyo wanajiandikisha kwa mfumo wa TEHAMA, kulipa ada sambamba na kuhamasisha Wanawake wengine wajiunge na UWT.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Serengeti, Jacob Bega akizungumza na Wajumbe wa baraza hilo amesema, jumuiya hiyo ilishiriki vyema kukiletea ushindi wa kishindo wa kata zote za Wilaya ya Serengeti na jimbo ikishirikiana na jumuiya zingine ndani ya chama hicho katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 huku akiwahimiza kutotumiwa vibaya na watu wenye nia ovu bali wadumishe amani, umoja na mshikamano kwa masilahi mapana ya jumuiya hiyo na Chama Cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Serengeti, Ester Mung'ori akizungumza katika kikao cha Baraza la UWT Wilaya ya Serengeti kilichohudhuriwa na Mjumbe wa baraza la UWT Taifa Mkoa wa Mara, Rhobi Samwelly na viongozi wa Wilaya hiyo.
"UWT ni jumuiya muhimu kwa maendeleo ya Chama Cha Mapinduzi, niwaombe mdumishe amani kuanzia ngazi za familia na ndani ya chama msikubali kutumika hata kidogo. Amani ikitoweka kinamama na Watoto watapata shida kubwa, niwasihi muendelee kukipigania chama kwa nguvu zote ikiwemo kuongeza wanachama wapya katika maeneo yenu," amesema.

Mbali na hayo, amewaomba kuendelea kufanya kazi za maendeleo kwa bidii na kutumia fursa ya mikopo ya asilimia 4 kati ya 10 ambazo hutolewa kusaidia vijana, Wanawake na watu wenye ulemavu katika Halmashauri. Huku pia akiwataka wajiepushe na baadhi ya watu wanaohamasisha uvunjifu wa amani kwa kisingizio cha kudai Katiba mpya ambapo amesema amani ikitoweka Maendeleo hayatafanyika
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Serengeti, Jacob Bega akizungumza katika kikao cha Baraza la UWT Wilaya ya Serengeti kushoto kwake ni Mjumbe wa Baraza la UWT taifa Wilaya ya Serengeti, Rhobi Samwelly na kulia Ester Mung'ori, Mwenyekiti wa UWT Serengeti.

Awali akifungua kikao hicho, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Serengeti, Ester Mung'ori amesema kuwa, jumuiya hiyo itaendelea kusimama imara kuhakikisha chama kinaendelea kufanya vizuri katika chaguzi zijazo na kuendelea kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii Wananchi

Katika kikao hicho, wadau mbalimbali wa Maendeleo wa Wilaya ya Serengeti ambao wamekuwa wakiisaidia jumuiya hiyo wamekabidhiwa vyeti na jumuiya hiyo kwa lengo la kutambua na kuthamini mchango wao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news