TAARIFA YA HALI YA HUDUMA YA MAJI OKTOBA 3, 2021 JIJINI MWANZA


Tumepokea taarifa kutoka TANESCO kwamba Tarehe 03 Oktoba, 2021 (Jumapili) kuanzia Saa 1:00 Asubuhi hadi Saa 11:00 Jioni watazima umeme (Mkoa wa Mwanza) ili kupisha maboresho ya miundombinu yao.

Hivyo basi, Vituo vyote vya kusukuma maji (Jiji la Mwanza, Nansio, Magu na Misungwi) havitofanya kazi hadi hapo maboresho ya TANESCO yatakapokamilika.

Kwa muda wote huo hakutakuwa na uzalishaji wa maji na hivyo maeneo yote yanayohudumiwa na MWAUWASA (Jiji la Mwanza na viunga vyake, Misungwi, Nansio, Ngudu na Magu) yataathirika.

Tunawasihi kuanzia sasa kuhifadhi maji yatakayotumika wakati wote wa maboresho ya TANESCO.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza, huduma itarejea katika hali ya kawaida baada ya nishati ya umeme kurudi.

Imetolewa na:-

Kitengo cha Uhusiano MWAUWASA

30/09/2021

_Upatapo taarifa hii, tafadhali mfahamishe na mwingine_

☎️0800110023

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news