Tanga Yemen Society for Charity yawafikishia wanafunzi maji

Na Hadija Bagasha, Tanga

TAASISI ya Kiislamu ya Tanga Yemen Society for Charity (TYSC) imezindua kisima chake cha kwanza cha msaada walichokijenga katika shule ya Sekondari ya Tanga School aliyosoma Rais wa Awamu ya Nne Dkt.Jakaya Kikwete, ambacho kitakasaidia kumaliza tatizo la uhaba wa maji ambao ulikuwa ukiwakabili hapo awali.
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Abdulrahman Shiloo wakati akizindua kisima katika Shule ya Tanga Ufundi kilichojengwa na Taasisi ya Kiislamu ya Tanga Yemen Society for Charity (TYSC), na kufadhiliwa na Fathhiya Foundation ya Moshi. (Picha na Hadija Bagasha).

Shule hiyo yenye wanafunzi wapatao 1,174, wanahitaji matumizi makubwa ya maji kwa mahitaji ya kila siku na kabla wana matenki ya lita 30 huku maji ya Tanga-Uwasa yakitumika jikoni.

Awali akizindua kisima hicho, Meya wa Jiji la Tanga, Abdulrahman Shiloo, kilichofadhiliwa na Fathhiya Foundation ya Moshi, alisema halmashauri itawaunga mkono katika jituhada zao za malengo yakusaidia jamii Jijini hapa na Tanga kwa ujumla.
"Niwahakikishie kwamba baraza letu la madiwani la Halmashauri ya Jiji, litawaunga mkono katika malengo yenu na inawatia moyo muwe chachu ya kusaidia jamii ya wana-Tanga," amesema Meya Shilow.

Awali Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Abdallah Said Bazar alisema kisima hicho ni cha kwanza tangu waianzishe taasisi yao baada ya kuombwa na wanafunzi wanaoswali katika msikiti uliopo shuleni hapo.
"Mheshimiwa Mstahiki Meya, kisima hiki ni cha kwanza tangu tuanze kufanya kazi, na huu ni mwanzo bado mipango na malengo yetu ni kusaidia jamii zaidi katika miradi ya maendeleo kwa jamii yetu," amesema Mwenyekiti huyo.

Naibu Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Ahmed Basalama, alisema taasisi hiyo itajikita zaidi katika kusaidia majanga ya moto, kusaidia vituo vya kulelea watoto yatima pamoja na kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu.

Hata hivyo, alisema taasisi hiyo iliyokuwa na kituo cha kufundisha watoto barabara ya nane, imepanga malengo ya muda mrefu kujenga hospitali na shule.

"Taasisi yetu katika malengo ya baadae tumepanga kujenga hospitali, shule na tutakuwa na kliniki ya masuala mbalimbali kwa watu wenye shida, "amesema Naibu Katibu huyo na kugusia kwamba hivi karibuni wanatarajia kuanzisha darasa la kufundisha kompyuta.
Mkuu wa shule ya Tanga Ufundi, Andrew Mwakanyamale, alishukuru kwa msada wa kuchimbiwa kisima hicho ambacho kitaongeza idadi ya vyanzo vya maji katika jumuiya ya shule hiyo.

Alisema shule hiyo yenye wanafunzi wapatao 1,174, wanahitaji matumizi makubwa ya maji kwa mahitaji ya kila siku na kabla wana matenki ya lita 30 huku maji ya Tanga-Uwasa yakitumika jikoni.

"Uzinduzi wa kisima hiki utatusaidia katika maeneo yetu mengi ya jumuiya ya shule na hasa hapa msikitini na mabweni yaliyokuwa karibu, "amesema mwalimu huyo.

Taasisi hiyo, inayoendeshwa na Watanzania na watu wa Yemen, imeanzishwa hivi karibuni ikiwa na lengo la kusaidia jamii ikiwemo kutoa elimu ya dini ya kiislamu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news