Wafanyakazi saba raia wa Afrika Kusini wadakwa ndani ya Tanga Cement

Na Hadija Bagasha, Tanga

Wafanyakazi saba raia wa Afrika Kusini wa kiwanda cha Saruji Tanga (Tanga cement) wamekamatwa na Idara ya Kazi mkoani Tanga kwa kosa la kukutwa wakifanya kazi bila kibali.
Janeth Omolo ambaye ni Afisa Kazi Mfawidhi Mkoa wa Tanga akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake (hawapo pichani).

Wafanyakazi hao wamekamatwa katika operesheni maalumu iliyofanywa na idara hiyo ambayo inaeendelea kwenye viwanda mbalimbali ikiwemo Tanga Cement.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Afisa Kazi Mfawidhi Mkoa wa Tanga, Janeth Omolo amesema wafanyakazi hao wamekamatwa Septemba 3, mwaka huu katika operesheni hiyo.

Omolo amewataja wafanyakazi hao ambao ni raia wa Afrika Kusini kuwa ni Caspurus van Niekerk/Supervisor, Charles Andre Thomson/Boilemaker,Keith Randall/Fitter, John James Pienaar/Electrician,Jan Andries Vander West thuizen/Boiler maker,Charles Albart Edwin/Electrician, na Francois Kleyn/Fitter,tunner.

Omolo amesema, kwa mujibu wa sheria ya kuratibu ajira za wageni namba 1, 2015 raia wote wa kigeni wanaoajiriwa na kufanya kazi nchini wanatakiwa kupata kibali cha Kamishina Mkuu wa Kazi na kueleza kuwa kazi yao ni kusimamia sheria ya kazi sura 366 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

“Raia hawa saba wa South Africa tumewakamata kwa kuwa tumebaini wapo na wanafanyakazi hapa nchini bila kibali na baada ya kugundua hilo tulitoa taarifa polisi na kufungua kesi Chumbageni na utaratibu mwingine unaendelea ili tuweze kuwafikisha mahakamani,”alisisiza Omolo.

Waajiri wote Tanga wanatakiwa kuhakikisha wanapoajiri raia wa kigeni wanafuata sheria za nchi, sheria ya kuratibu vibali sheria namba 1 mwaka 2015 ili kutekeleza sheria hizo bila shuruti kwani kumuajiri mfanyakazi bila kuwa na kibali cha kazi ni kosa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha sheria ya kuratibu ajira za wageni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news