Yanga SC yawachezesha kwata Rivers United, alama zote tatu zaelekea Lagos

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Licha ya Yanga SC kuwachezesha wageni wao soka safi.Ushindi wa alama tatu umeelekea Lagos, Nigeria.

Ni kupitia mechi ya mkondo wa kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali kati ya Yanga SC ya Tanzania dhidi ya Rivers United FC ya Nigeria.

Mtanange huo umemalizika kwa Rivers United kushinda goli 1-0 na kuondoka na alama zote tatu.
Katika mchezo huo ambao umepigwa leo Jumapili Septemba 12,2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam, timu zilitoshana nguvu katika dakika 45 za kwanza.

Katika kipindi cha pili timu zilianza kwa kushambuliana kwa zamu kabla ya Rivers United kupata goli la kuongoza kupitia kwa Moses Omoduemuke dakika ya 51.

Aidha,baada ya mchezo huo wa kwanza sasa mchezo wa mkondo wa pili utapigwa nchini Nigeria wiki mbili zijazo.

Post a Comment

0 Comments