BARAZA LA MAWAZIRI WA AFRIKA WANAOSIMAMIA BIASHARA, WA AFCFTA WAKUBALIANA BAADHI YA VIGEZO VYA UASILI WA BIDHAA

NA MWANDISHI MAALUM

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (MB) ameshiriki Mkutano wa 7 wa Baraza la Mawaziri wa Afrika wanaosimamia Biashara, wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) uliofanyika kwa njia ya kawaida na mtandao (hybrid) tarehe 10 Oktoba 2021) ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mtumba.
Mawaziri hao walipitia hatua iliyofikiwa katika masuala mbalimbali yaliyomo katika Awamu ya Kwanza ya Majadiliano, ambayo bado hayajakamilika na kufanya maamuzi. Aidha wametoa muda wa miezi mitatu kwa wataalam kukamilisha maeneo ambayo hayajakamilika ili kukamilisha majadiliano hayo kwa asilimia 100

Aidha Mawaziri hao walikubaliana baadhi ya vigezo vya uasili wa bidhaa na kufanya vifikie asilimia 88.1 kutoka asilimia 86.03 ya awali ikiwemo vigezo vya uasili wa bidhaa za Maziwa (cheese and curd), Juisi za matunda (Cranberry juice, mixture of juices), na vifaa vya bidhaa za ngozi (Articles of leather).

Tanzania imeridhia Mkataba wa AfCFTA ambao hadi sasa jumla ya nchi 38 kati ya nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika zimeridhia Mkataba huo huo ulianza kutekelezwa rasmi tarehe 30 Mei, 2020. Jumla ya nchi 41 zimewasilisha mapendekezo ya tariff offer kwa ajili ya kuanza kufanya biashara. Kati ya nchi hizo, zipo jumuiya nne (4) za Umoja wa Forodha ambazo ni Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC), Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (CEMAC), Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na Umoja wa Forodha Kusini mwa Afrika (SACU).

Prof. Mkumbo amesema,Tanzania inatarajia kunufaika na kutumia fursa zote za kibiashara zinazotokana na Makataba huo ikiwemo kupatikana kwa masoko mapya ya mazao ya kilimo yatakayochochea uzalishaji, kuimarika kwa mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo yanayohusisha wakulima wadogo kama vile alizeti, pamba, karafuu, viungo, matunda na mbogamboga kutokana na kuongezeka kwa soko la bidhaa zitakazozalishwa nchini

Kuongezeka kwa uzalishaji na ajira kwa wakulima na wadau wanaohusika katika mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo, kupatikana kwa soko kubwa la bidhaa na huduma lenye idadi ya watu takriban bilioni 1.2 ukilinganisha na idadi ya watu takribani milioni 522 katika nchi za EAC na SADC, kuongezeka kwa tija na ubora kwa bidhaa na huduma za Tanzania kutokana na kuongeza kwa ushindani na hivyo kupelekea kupungua kwa bei za bidhaa,"ameongeza Prof. Mkumbo.

"Faida nyingine za kuridhia mkataba huo ni pamoja na na Kuimarisha ushirikiano wa kibiashara sambamba na kuviendeleza viwanda na wajasiriamali kundi la Wajasiriamali wodogo sana, Wadogo na wa Kati (MSMEs), Upatikanaji wa bidhaa za aina mbalimbali (varieties) nchini na Uhawilishaji wa teknolojia kutoka nje ya nchi (technology transfer) kutokana na uwekezaji utakaofanyika nchini,"amesema Prof. Mkumbo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news