Bernard Membe afunguka kuhusu Rais Samia, asisitiza anatosha

NA MWANDISHI MAALUM

Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amesema Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi jasiri na mahiri, anatosha kuiongoza Tanzania na anamuunga mkono kwa kazi kubwa anayoifanya.
Membe ameyasema hayo leo Oktoba 5, 2020 alipozungumza mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo Mkoani Lindi.

Membe amemuomba Waziri Mkuu afikishe salamu zake pamoja na za wananchi wa kijiji cha Rondo kwa Mheshimiwa Rais Samia kwamba wanamuunga mkono katika jitihada kubwa za kuwaletea wananchi maendeleo.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba ufikishe salamu zetu sisi Wana-Rondo kwa Mheshimiwa Rais Samia mwambie tunampenda, anatosha na tutamsaidia,” alisema Membe.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Rondo, Waziri Mkuu amewasihi wananchi hao wawapeleke watoto shule, kuanzia ngazi ya elimu ya awali na shule za Sekondari kwani Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na mama Samia Suluhu Hassan imeweka msisitizo katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu bora.

Aidha, Waziri Mkuu ametoa onyo kali kwa vijana na watu ambao wamekuwa wakiwarubuni wanafunzi wa kike kuacha masomo na wengine kuwapa mimba waache ili watoto hao waweze kutimiza ndoto zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news