Chama cha Maafisa Uhusiano na Umma Tanzania (PRST) wana jambo kubwa Dar

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Chama cha Maafisa Uhusiano na Umma Tanzania (PRST) kimewaalika wadau wake kwenye mkutano mkuu wa kwanza wa mwaka utakaofanyika kesho Oktoba 28 hadi Oktoba 29, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Rais wa chama hicho, Loth Makuzi ametoa wito huo katika mkutano na waandishi wa habari ambao umefanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Makuzi amesema, Mkutano wa Mkuu wa chama hicho utafanyika Oktoba 28 na 29, 2021 jijini Dar es Salaam ambapo washiriki mbalimbali kutoka Tanzania na nje ya Tanzania wanatarajiwa kuhudhuria.

Amesema, chama hicho kinatarajia kupokea ugeni kutoka nchini Kenya na Afrika Kusini ambapo marais wa vyama vyao vya Maafisa Uhusino wa Umma katika nchi zao wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo na pia kutoa mada.

Makuzi akifafanua zaidi kuhusu mkutano huo amesema, mgeni rasmi katika mkutano huo wa siku mbili anatarajiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt.Jim Yonazi.

Ameongeza kuwa, katika mkutano mkuu wa chama hicho yatafafanuliwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujadili changamoto na mafanikio ya chama hicho ambapo pia amewakaribisha wadau wote katika tasnia hiyo kwa ajili ya kuijadili na kutafuta ufumbuzi pale ambapo kutawasilishwa changamoto.

Makuzi amesema, mkutano huo utawahusu wadau wote wa habari, maafisa mahusiano, mawasiliano, masoko na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambapo kutakuwa na mjadala mpana kuangalia na kutatua changamoto zinazoikabili tasnia hiyo.

“Hatujawahi kufanya mkutano mkubwa kama huu, huu ni mkutano wa watu wote, waandishi wa habari, watu wa mahusiano, mawasiliano, masoko na TEHAMA,tutakuwa na mijadala mipana kuijadili taaluma na kuitetea,”amesema Makuzi.

Amesema, mkutano huo pia unalenga kujenga mahusiano mazuri kati ya waandishi wa habari na maafisa uhusiano kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali katika taasisi na jamii kwa ujumla.

“Mkutano huu utajadili pia masuala mtambuka ya tasnia hii, kuangalia wapi tumeanguka na namna gani tufanye ili tuboreshe mazingira na kutoa kilicho bora kwa jamii,"amesema Makuzi.
Naye Katibu Mkuu wa PRST, Ndege Makura amesema kuwa, kwa muda jumuiya hiyo imeshindwa kufanya mikutano miwili ya mwaka kutokana na mlipuko wa virusi vya korona (Uviko-19).

"Huu utakuwa ni Mkutano Mkuu wa kwanza tangu tuanzishe Chama cha Maafisa Uhusiano kwa Umma Tanzania mwaka 2017 na kuanza kazi mwaka 2018,"amesema.

Amesema, mkutano huo pia unalenga kujenga mahusiano mazuri kati ya waandishi wa habari na maafisa uhusiano kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali katika taasisi na jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mary Kafyome ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mkutano huo amesema kuwa,mkutano huo wa mwaka utakuwa ni mpango mzuri kwa wadau na pia utajenga mahusiano mazuri kati ya wanahabari na maofisa mahusiano.

Pia amesema kuwa, mkutano huo wa siku mbili pia itajadili masuala mtambuka katika tasnia ya habari, waandishi wa habari na maafisa habari pamoja na kuchagua viongozi wapya wa PRST.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news