Dkt. Abbasi aongoza mapokezi Twiga Stars

Na Mwandishi Wetu

Serikali imewaahidi wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars), kuwapa zawadi itakayoonesha thamani ya heshima waliyoliletea Taifa baada ya kutwaa ubingwa wa Cosafa nchini Afrika Kusini.

Hayo yamesemwa Oktoba 11, 2021 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, aliyeiwakilisha Serikali kuipokea timu hiyo usiku huu.

“Siku ile tunawaaga mliahidi ubingwa leo mmetimiza ahadi yetu na mmerejea mkiwa mashujaa wa Taifa. Sasa kazi iko kwetu kuwaenzi na Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan ameshawapongeza na ameahidi atawaenzi na kutambua mchango wenu sasa tusubiri ahadi yake,”amesema Dkt.Abbasi.

Wakati Serikali na wadau wengine wakiendelea kuipongeza timu hiyo, Dkt. Abbasi amesema Oktoba 12, 2021 wachezaji hao wataandaliwa chakula maalum cha jioni jijini Dar es Salaam ambapo Serikali na wadau watatangaza zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa timu hiyo.

Post a Comment

0 Comments