Joseph Mgongolwa: Dkt.Abel Nyamahanga anazidi kurejesha heshima ya CCM mkoani Iringa

NA MWANDISHI MAALUM

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Iringa Mjini, Joseph Mgongolwa amempongeza Mwenyekiti wa chama hicho mkoa, Dkt. Abel Nyamahanga kwa kuja na ubunifu ambao umelenga kukiimarisha chama kuanzia ngazi za shina hadi ngazi za juu.
Mgongolwa ametoa pongezi hizo baada ya Dkt. Abel Nyamahanga kuanza ziaza ya kata kwa kata na baadaye wilaya kwa wilaya ambayo imeonyesha mafanikio makubwa.

"Ubunifu wa Dkt.Abel Nyamahanga ni wa kupongeza sana na hii ni hatua nzuri ambayo inadhirisha wazi kuwa, amedhamiria kwa dhati kuijenga CCM mpya ambayo ina maono shirikishi na niseme wazi kuwa Dkt. Nyamahanga anafanya kazi nzuri inayolenga kumsaidia Mwenyekiti wa chama Taifa, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kulisongeza mbele kurudumu hili la kukistawisha chama na anazidi kurejesha heshima ya chama Iringa.

"Niendelee kusisitiza kuwa, sisi pia wanachama, makada na viongozi wa mkoa huu tutaendelea kushirikiana naye bega kwa bega kuhakikisha kuwa, CCM inazidi kuwa baba lao, hakuna ubishi kuhusu ukubwa, nguvu na umuhimu wa chama hiki katika kuwatumikia Watanzania kwa misingi ya umoja, haki, upendo na mshikamano, hivyo tunaendelea kukisimamia chama hiki mchana na usiku ili kizidi kuwa nuru kwa Watanzania,"amefafanua Mgongolwa.

Dkt. Abel Nyamahanga amekuwa na ziara za kukijenga chama hicho kuanzia kata kwa kata ambapo kwa sasa anaendelea katika wilaya ya Kilolo.
Aidha, Mgongolwa ametoa pongezi hizo ikiwa naye ni miongoni mwa wabunifu wa mikakati mbalimbali ya kuwaleta pamoja wana CCM mjini hapa ili kuhakikisha wanaendelea kujiunga na chama na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Pia amekuwa mstari wa mbele kuyajengea makundi mbalimbali ya vijana, wanawake uwezo ili kujikwamua kiuchumi, hatua ambayo inaunga mkono harakati za Serikali za kuyakomboa makundi mbalimbali katika jamii kiuchumi.

Amesema, jitihada hizo anazifanya ilim kuunga mkono kazi nzuri zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa katika kuwainua Watanzania kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news