Kafulila awavua uongozi vigogo 18 wa AMCOS Maswa

Na Derick Milton,Maswa

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila amewavua uongozi, viongozi 18 wa vyama vya msingi vya ushirika wilayani Maswa mkoani humo kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa pesa za wakulima sh.milioni 68 msimu wa pamba uliopita wa mwaka 2020/2021.
Mbali na kuwavua uongozi, Mkuu huyo wa Mkoa ametoa siku 14 kwa viongozi hao ambao wanatuhumiwa, kuhakikisha ndani ya kipindi hicho wanarejesha kiasi hicho cha pesa ambacho ni jasho la wakulima.

Kafulila ametoa maamuzi hayo wakati wa kikao chake na wadau wa pamba wilayani humo ambacho kilikuwa maalumu kujadili mpango mkakati wa mkoa katika kuongeza uzalishaji kwenye zao hilo msimu 2021/2022.

Amesema kuwa, kama kiongozi wa mkoa, hatoweza kuvumilia kuwa na viongozi ambao wanahujumu zao la pamba ikiwemo kuwaibia wakulima, na wala hatokuwa na aibu ya kuchukua hatua yeyote kwa mtu yeyote.

“Hatuwezi kuendelea kuwa na viongozi wa namna hii, kwanza kuanzia sasa hatakiwi tena kuwa viongozi wa Amcos kwenye maeneo yao, lakini ndani siku 14 wote wahusika wanatakiwa kuwa wameresha fedha hizo za wakulima,” amesema Kafulila.

Aidha, amemwagiza Ofisa ushirika wilayani humo kuhakikisha wanafanya utaratibu wa kupata viongozi wengine wapya ili shughuli za ushirika ziweze kuendelea na kuhakikisha pesa hizo za wakulima zinarejeshwa.

“Kupitia mpango huu, viongozi ambao siyo waadilifu hawana nafasi hata kidogo, tutachukua hatua kali kwa Amcos ambazo zimekuwa na vitendo vya wizi kwa wakulima wake, na hawa ambao tumewasimamisha leo, wakishindwa kurejesha kwa siku hizo 14, watataifishwa mali zao,” amesema Kafulila.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo, Aswege Kaminyonge alisema kuwa bodi ya pamba imeendelea kuleta mbegu kwa wakulima, huku akibainisha uwepo wa kasi ndogo ya wakulima kununua mbegu na Wilayani mahitaji ni tani 3,000 na tayari wamepokea tani 700 tu.

Naye Mwakilishi wa Kampuni ya kuchambua pamba Alliance Ginery kutoka Bariadi, Ernest Edward ameilalamikia bodi ya pamba kutokana na ucheleweshaji wa mbegu hali inayopelekea magari kukaa muda mrefu bila kupakia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news