Maagizo ya Rais Samia kwa viongozi baada ya kufanya uapisho Ikulu leo

NA GODFREY NNKO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb) kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Pauline Philipo Gekul (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Eng. Kundo Endrea Mathew (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Jaji Jacob Casthom Mwatembela Mwambengele kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Samia amesema hayo leo tarehe 24 Oktoba, 2021 mara baada ya kuwaapisha viongozi hao katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Amesema uteuzi wa viongozi hao utaleta uwajibikaji mzuri hasa katika sekta ya Habari na Mawasiliano kwasababu hivi sasa inakwenda kwenye mabadiliko ya kukuza matumizi ya teknolojia na kuwataka viongozi hao kuwajibika katika nafasi zao hizo ili Tanzania ipige hatua kimaendeleo.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amewataka viongozi mbalimbali walioteuliwa akitolea mfano Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na kuacha mara moja mivutano isiyo na tija katika majukumu yao.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amempongeza Mhe. Rais Samia kwa jitihada zake anazozifanya na hivi sasa kuna miradi mingi inayotekelezwa katika sekta mbalimbali ikiwemo ya michezo ambayo hivi sasa inafanya vizuri ndani na nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Magdalena Kamugisha Rwebangira kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndugu. Asina Abdallah Omar kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb) wa kwanza kulia, Naibu Waziri Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Philipo Gekul (Mb), Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Eng. Kundo Endrea Mathew (Mb) Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jacob Casthom Mwatembela Mwambengele, Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Magdalena Kamugisha Rwebangira na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu. Asina Abdallah Omar wakila kiapo cha Maadili ya Utumishi wa umma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kumuapisha Waziri, Naibu Mawaziri katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali haina wasiwasi nayo kwasababu watendaji wa Tume hiyo wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Aidha, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Akson, amewataka viongozi wa Tume ya Uchaguzi kuwa na utaratibu wakufanya matayarisho ya uchaguzi mapema, badala ya kusubiri hadi uchaguzi unapofika ili kuepuka malalamiko kutoka kwa wanasiasa dhidi ya Tume hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye wakizungumza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021 wakati wa Mhe. Ndayishimiye alipokua akiondoka kurejea Nchini Burundi baada ya kukamilisha ziara yake hapa Nchini.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021 mara baada ya Rais huyo wa Burundi Mhe. Ndayishimiye kuhitimisha zira yake nchini na kurejea Burundi.

Wakati huohuo, Mhe. Rais Samia amewaongoza viongozi mbalimbali kumuaga Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku tatu hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mke wa Rais Evareste Ndayishimiye wa Burundi kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021 wakati Mhe. Ndayishimiye alipokua akiondoka kurejea Nchini Burundi baada ya kukamilisha ziara yake leo tarehe 24 Oktoba, 2021. kulia ni Rais wa Ndayishimiye wa Burundi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021 wakati Mhe. Ndayishimiye alipokua akiondoka kurejea Nchini Burundi baada ya kukamilisha ziara yake leo tarehe 24 Oktoba, 2021. (PICHA ZOTE NA IKULU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news