Mwalimu Mkuu ampiga hadi kumng'oa jino Mwalimu mwenzake

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mkuyuni iliyopo katika Tarafa ya Mkuyuni Morogoro Vijijini anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kumpiga hadi kumng'oa jino la juu mwalimu mwezake, Witnes Makoti huku chanzo kikiwa bado hakijulikani.
Mwalimu huyo aliyefahamika kwa jina la Mussa Hasira anadaiwa kutenda tukio hilo Oktoba 15,2021 baada ya kupishana kauli wakiwa shuleni hapo

Kamanda wa Polisi wa Polisi Morogoro, Fortunatus Musilimu ametbibitisha kushikiliwa kwa mtuhumiwa.

Amesema kuwa, mtuhumiwa huyo alimshambulia kwa fimbo na ngumi mwalimu mwenzake huyo hadi kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili.

Post a Comment

0 Comments