Mwenge Maalum wa Uhuru 2021 wapokelewa Bukombe

NA MWANDISHI MAALUM

WAKAZI wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita wameupokea Mwenge wa Uhuru wa Kitaifa ukitokea mkoani Kagera ambapo Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule amemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Said Nkumba kwa ajili ya kupitia miradi 10 ya halmashauri hiyo.
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko akiwa amebeba Mwenge Maalum wa Uhuru 2021 na viongozi wengine katika Jimbo la Bukombe mkoani Geita.

Miongoni mwa viongozi waliokuwepo wakati Mwenge Maalum wa Uhuru 2021 ukipitia miradi ya elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara ni Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo.

Miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja imetembelewa na Mwenge wa Uhuru wa kitaifa.
Kiongozi wa Mwenge Maalum wa Uhuru 2021, Luteni Josephine Mwambashi akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wa Jimbo Bukombe mkoani Geita leo Oktoba 9, 2021.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi ameongoza wakimbiza Mwenge wa Uhuru kukagua na kutembelea miradi hiyo.

Kesho mbio za Mwenge wa Maalum wa Uhuru zinatarajiwa kupokelewa Wilaya ya Mbogwe ambapo unaongozwa na kauli mbiu ya ‘TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu itumike kwa usahihi na uwajibikaji”.

Post a Comment

0 Comments