KCB YANUFAISHA VIJANA 504 ELIMU YA UJASIRIAMALI

NA ISSA MOHAMED, DAR ES SALAAM

Takribani vijana 504 katika mikoa mbalimbali nchini, wamefadika wameondokana na dhana ya kusubiri kuajiriwa huku vijana 304 wakiwa tayari wamefuzu masomo –Veta na mafunzo ya ujasiriamali kupitia Programu ya 'KCB 2jiajiri Youth Empowerment' iliyoanzishwa na benki hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Masoko, Uhusiano na Mawasiliano wa Benki hiyo, Christina Manyenye, alisema shabaha ya kuanzisha programu hiyo ni kufungua fursa kwa vijana.

Alibainisha katika vijana hao zaidi ya wanawake 356 wamefaidika kwa mafunzo darasani kwa vitendo katika vyuo mbalimbali vya Ufundi Stadi (VETA).

Mbali na vijana hao, alieleza Oktoba 18, mwaka huu wengine 200 wanatarajiwa kuanza masomo ili kunufaika na programu hiyo, huku lengo likiwa ni kuwafikia vijana 4,000 nchini.

"Ukiangalia tangu tumeanza programu hii mwaka 2016 wanawake 356 wamenufaika na mafunzo darasani na vitendo," alisema.

Alifafanua kupitia programu hiyo, vijana wanafundishwa ujasiriamali, namna ya kutunza kumbukumbu za fedha na biashara zao, kadhalika mbinu za kutafuta masoko.

"Katika hawa pia wapo wanawake walionufaika na ruzuku ya sh. milioni tano kwa kila mmoja ili kuendeleza biashara zao," alisema Christina.

Aidha, alieleza kwa sasa programu hiyo inafanyika katika maeneo mbalimbali nchini vikiwemo visiwa vya Zanzibar, Morogoro, Arusha, Dar es salaam, Mwanza na Moshi.

Kuhusu mchango wa Benki hiyo kwa serikali, Christina aliweka wazi kwamba tangu kuanzishwa kwake imeweka takribani sh. bilioni 63 kama mtaji.

"Benki ya KCB imekuwa na mwenendo mzuri wa ulipaji kodi ambapo kwa mwaka inakadiriwa kulipa kodi ya sh. bilioni13,"alieleza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

Previous Post Next Post

International news