Radi yaua ng'ombe 15 wakiwa zizini

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Zaidi ya ng'ombe 15 wamekufa baada ya kupigwa na radi katika Kijiji cha Mwibiti kilichopo Kata ya Ikomwa Manispaa ya Tabora mkoani Tabora.
Katika tukio hilo kati ya ng'ombe 30 waliokuwa kwenye zizi moja 15 kati yao wamepigwa na radi usiku wa kuamkia leo Oktoba 18,2021 na kufa.

Ng'ombe hao wanamilikiwa na mfugaji wa kijiji hicho, Nhomano Lugwesa.

Aidha, Serikali ya wilaya ikiongozwa na mkuu wa Wilaya ya Tabora, Dkt. Yahya Nawanda, imefika katika eneo la tukio kwa lengo la kuwapa pole wanafamilia.

Hata hivyo, kufuatia hali hiyo serikali imeahidi kufanya tathmini kwa ajili ya kumshika mkono mfugaji huyo.

Post a Comment

0 Comments