Rais Samia afanya uteuzi

NA GODFREY NNKO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, amemteua Bw. Mustafa Hamisi Umande kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Chai Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. (Picha na Maktaba).

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa Oktoba 11, 2021 na Jaffar Haniu ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Bw. Umande anachukua nafasi ya Mhandisi Steven D. Mlote ambaye amemaliza muda wake.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, uteuzi huo umeanza Oktoba 8, 2021.

Post a Comment

0 Comments