RC Mtaka: Msipandishe bei vifaa vya ujenzi, zingatieni bei elekezi ya Serikali

Na Doreen Aloyce, Diramakini Blog

WAFANYABIASHARA wa vifaa vya ujenzi mkoani Dodoma wametakiwa kuacha kupandisha bei za bidhaa zao badala yake wametakiwa kuuza kwa kizingatia bei elekezi ya serikali.

Hatua hiyo inakuja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kupokea fedha za mkopo nafuu kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa ajii ya kupambana na ugonjwa wa Corona ambapo mkoa wa Dodoma umepokea jumla ya shilingi Bilioni 17.97 kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza na wafanyabishara hao, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amesema fedha hizo ni fursa kubwa kiuchumi kupitia biashara kwani fedha hizo zinakwenda kwa wafanyabiashara wazalendo wakiwemo wa kati na wadogo ili kuwainua.

Amesisitiza fedha hizo zimetolewa lengo ni kwenda kuwanufaisha sekta binafsi na wafanyabiashara wadogo na wakati hivyo ni marufuku bidhaa za ujezi kupandishwa bei kiholela.

"Na endapo ikatokea au kujulikana nyinyi wafanyabishara mmepandisha bei kiholela serikali ya mkoa itakwenda kununua bidhaa na vifaa vya ujenzi mikoa mingine," amesema Mtaka.

Pia amesema kupitia fedha hizo sekta binafsi inakwenda kukua na hata uchumi wa mtu mmoja mmoja kwani kupitia fedha hizo kila kata imepitiwa na ujenzi wa miradi ya kimaendeleo.

"Sasa niwaombe wafanyabiashara fedha zimetufikia sasa tusilale tuchangamke,soko hilo masuala ya kulala unafungua duka saa sita mchana msije kumtafuta mchawi," amesema mkuu wa mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo amesema, fedha hizo ni fursa kubwa kwenye uchumi kupitia biashara kwani fedha hizo zinakwenda kwa wafanyabiashara wazalendo wa kati na wadogo.

"Nataka mtambue kwamba fursa zinazokuja lengo tunataka kuzalisha wafanyabishara mamilionea na mabilionea, kupitia fedha hizi tunataka wafanyabishara wadogo wakue kikubwa tubadilishe bishara zetu,"amesema.

Sambamba na hilo waziri huyo amewataka wafanyabiashara hao kuzingatia mambo makuu matatu amabayo ni kutosheleza mahitaji kama ni kukopa mikopo waende kukopa fedha kwenye taasisi za kifedha kwani soko lipo la kutosha na waache imani za kishirikina.

Suala la pili ni kuzingatia ubora, Waziri huyo amesema kumekuwepo na shida panapokuwa na mahitaji makubwa wafanyabishara wamekuwa wakichukua bidhaa bila kuzingatia ubora sasa kipindi hiki watafuatilia ubora.

Na jambo la tatu ni kuzingatia maadili ambapo amewataka wafanyabiashara hao kusimama imara kwa kuuza bidhaa na kutoa risti tena ya mashine ya Efd.

Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma, Dkt.Fatuma Maganga amewataka wafanyabiashara hao kuweka bidhaa zenye ubora na wazinagatie mahitaji na matakwa ya jiji linavyotaka kwani kila halmashauri inalangizake kwenye uezekaji wa mabati.

Naye mfayabishara Abdullah Taratibu ambaye ni Mratibu wa vijana wafanyabisharamkoa wa Dodoma TCCAI ameuomba uongozi wa mkoa kutoa ruhusa siku za Jumamosi wafanyabiashara wote wafungue masuka yao mapema.

"Ni kweli fursa ya fedha katika mkoa wetu zimetufikia,lakini na sisi wafanyabishara biashara tunabanwa kufanya biashara siku ya Jumamosi kutakiwa kufungua maduka saa 4 wakati siku ya Jumamosi ndio siku kubwa ya biashara,"amesema kiongozi huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news