Sarah Magesa: Watanzania tuzidi kumngoja Mungu katika nyakati zote za maisha yetu

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Watanzania wameombwa kuwa na tabia ya kumngoja Mungu katika vipindi mbalimbali ambavyo wanakutana navyo kila wakati katika maisha yao.

Hayo yamesemwa na Mwimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka Tanzania, Sarah Magesa kupitia wimbo wake mpya uitwao Bado Nakungoja.

Sarah amesema, kuna wakati Watanzania tunapitia vipindi vigumu na vingine vyepesi, kikubwa ni kuendelea kumngoja Mungu kwa Saburi.

"Ukiangalia kama nchi tunapitia vipindi tofauti vingine vinavunja Moyo na vingine vinaumiza kama wakati huu wa Ugonjwa wa Corona, tusiache kumtegemea na kumngoja Mungu atushindie,"amesema Sarah Magesa.
Wimbo wake Sarah Magesa uiitwao Bado Nakungoja umerekodiwa hivi karibu na ukiwa na ujumbe wa kuwasihi watu wote kuwa na tabia ya kumngoja Mungu katika mambo yote.

Post a Comment

0 Comments