STAMICO YAZINDUA VIFAA VYA KISASA VYA UCHIMBAJI MADINI

Tito Mselem na Bibiana Ndumbaro, Dodoma

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) linalenga kuimarisha shughuli na kuanzisha migodi yake yenyewe baada ya kununua vifaa vya uchimbaji na uchorongaji wa madini kwa kutumia vyanzo vyake vya ndani.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akikata utepe kuzindua magari na mitambo ya kisasa kwa ajili ya kuboresha shughuli za uchimbaji na uchorongaji wa madini unaotekelezwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila katika uzinduzi wa magari na mitambo ya kisasa kwa ajili ya kuimarisha shughuli za uchimbaji na uchorongaji wa madini.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akizungumza jambo kwenye kufunga kikao cha nane cha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kilichofanyika katika ukumbi wa Nishati jijini Dodoma.

Prof. Msanjila amesema vifaa vilivyozinduliwa vinaenda kuiwezesha STAMICO kuboresha utendaji kazi wake ambapo italiwezesha Shirika hilo kupata miradi mingine na kuitelekeza kwa ufanisi mkubwa.

"Ununuzi wa Mitambo hii utaiwesha STAMICO kutelekeza miradi na kandarasi mbalimbali iliyonayo pamoja na miradi mingine itakayo ipata ambapo itasaidia kuzalisha kwa faida na kutoa gawio kwa Serikali", amesema Prof. Msanjila.

Awali, Prof Msanjila alilifunga Baraza la 8 la wafanyakazi wa STAMICO na kuwataka wafanyakazi wote wa Shirika hilo kuendelea kushirikiana ili kufanikisha Malengo ya Shirika hilo.

Katika Baraza hilo, Prof. Msanjila amesema kuwa, makubaliano ya kikao hicho ni kufuatilia utelekelezaji wa malengo yaliyojadiliwa katika kikao kazi hicho na kusisitiza ufuatiliaji wa yote yaliyozungumzwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akikabidhi ufunguo wa mtambo wa kisasa ulionunuliwa na STAMICO kwa ajili ya kuboresha shughuli za uchimbaji na uchorongaji.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara na (STAMICO) mara baada ya kikao cha kufunga Baraza la nane la Shirika hilo kilichofanyika katika ukumbi wa Nishati jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakifuatilia kikao cha kufunga Baraza la 8 la wafanyakazi wa Shirika hilo kilichofanyika katika ukumbi wa Nishati jijini Dodoma.

Aidha, Prof. Msanjila amewataka watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la Sensa linalotarajia kufanyika Oktoba 2022 huku akiwahimiza watanzania wote kujitokeza kupata chanjo ya Uviko-19 kwani ugonjwa huu upo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwase ameeleza utekelezaji wa bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/2021 huku akizungumzia malengo ya kukusanya mapato kwa Mwaka wa Fedha 2021 kuwa, Shirika lilipangiwa kukusanya shilingi billion 19 .4 ambapo walivuka lengo kwa kukusanya bilioni 19.6 sawa na asilimia 101.
Baadhi ya washiriki walioshiriki kikao cha kufunga Baraza la 8 la wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakifuatilia Kikao kilichokuwa kinaendeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila.

Dkt. Mwase amesema, Shirika limeweza kununua magari na mitambo ya kisasa kwa ajili ya kuboresha shughuli za uchimbaji na uchorongaji wa madini ambapo kiasi cha shilingi bilioni 9.7 kilitumika.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Vanance Mwase akizungumza jambo kwenye kufunga kikao kazi cha Baraza la 8 la wafanyakazi wa Shirika hilo.

Dkt. Mwase ameongeza kuwa Shirika lina lengo la kujiimarisha zaidi katika kuendesha miradi yake na kutafuta zaidi kandarasi ili kijiongezea mapato na kulipa baadhi ya madeni ambayo Shirika ilikuwa inadaiwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara pamoja na viongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) katika uzinduzi wa magari na mitambo ya kisasa kwa ajili ya kuboresha shughuli za uchimbaji na uchorongaji jijini Dodoma.

Dkt. Mwase amesema, Shirika limeonesha viashiria vya kujiendesha kwa kujitegemea ambapo Shirika limepanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 76.2 kutoka vyanzo vyake vya ndani ambapo ndani ya miaka mitatu iliyopita Shirika lilikuwa linakusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.3, katika miaka mitatu iliyopita Shirika lilikuwa linaitegemea Serikali kwa asilimia 87 Mwaka wa Fedha 2021/2022 Shirika linaitegemea Serikali kwa asilimia 13.
Magari yaliyozinduliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila ili yakasaidie kuboresha shughuli za Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

"Shirika limepanga kununua mitambo 5 ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo ili tuweze kuwasaidia wachimbaji wadogo ambao sisi kama Shirika ndiyo walezi wao, na tuna mpango wa kuanzisha Vituo vingine viwili vipya vya Mfano ili kuiendeleza Sekta yetu ya Madini," amesema Dkt. Mwase.

Post a Comment

0 Comments