Tanzania, Kenya kumaliza vikwazo vya kiutawala Desemba 2021

NA MWANDISHI MAALUM

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kenya zimedhamiria kumalizia kuondoa vikwazo vya kiutawala vilivyosalia ifikapo Disemba, 2021 baada ya kuondoa vikwazo 46 visivyokuwa vya kikodi.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dany Kazungu akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi ndogo za wizara leo Jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa wakati wa mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dany Kazungu jijini Dar es Salaam ambapo takwimu zinaonesha urari wa biashara kati ya nchi hizo umeongezeka mara sita zaidi baada ya kuondolewa kwa vikwazo hivyo.

Kutokana na hatua hiyo, Tanzania imeonekana kunufaika zaidi kwa kuondolewa kwa vikwazo hivyo kwa kuuza zaidi bidhaa zake nchini Kenya.

“Hii ni ishara nzuri kwa Tanzania, lakini pia ni fursa kwa Tanzania na Kenya kuondoa umaskini kwa watoto wetu na ndugu zetu kupata ajira kwa wingi katika sekta ya biashara,”amesema Mhe. Kazungu.

Pia Balozi Kazungu amemueleza Waziri Mulamula kuhusu azma ya Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta kufanya ziara rasmi hapa nchini na kisha kuhudhuria sherehe za Uhuru tarehe 9 Disemba 2021 ambapo alialikwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipotembelea Kenya mapema mwaka huu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimuleleza jambo Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dany Kazungu walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za wizara leo Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe. Dany Kazungu yakiendelea katika ofisi ndogo za wizara leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema Tanzania inaheshimu makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa awali wa kuondo vikwazo hivyo na dhamira ni kuwa ifikapo Disemba 2021 vikwazo vya kiutawala navyo viwe vimeondolewa ili kukuza zaidi mahusiano ya Kidiplomasia na Biashara baina ya Tanzania na Kenya.

“Tumekubaliana kuhakikisha ifikapo mwezi Disemba 2021 vikwazo vyote vya kitawala viwe vimetatuliwa, azma yetu ni kuhakikisha kuwa kila kitu kinakuwa sawa kwa ustawi wa Diplomasia na biashara baina ya Tanzania na Kenya,” amesema Balozi Mulamula.

Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Mwakilishi wa Taasisi ya Sister Cities ya Marekani Bi. Ronda Pierce katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. Mwakilishi wa Taasisi ya Sister Cities ya Marekani, Bi. Ronda Pierce akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo za wizara leo Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo baina ya wakilishi wa Taasisi ya Sister Cities ya Marekani Bi. Ronda Pierce na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) yakiendelea katika Ofisi ndogo za Wizara leo Jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news