TANZIA:Profesa Mary Bernard Jande wa CUHAS-Bugando afariki

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi Mwambata (CUHAS-Bugando) jijini Mwanza ametangaza kifo cha Profesa Mary Bernard Jande.Kwa mujibu wa taarifa iliyoonwa na DIRAMAKINI BLOG, Profesa Mary Bernard Jande ambaye alikuwa Profesa katika Idara ya Clinical Pharmacology na Mkuu wa Kitivo cha Famasia mstaafu (2010-2018) amefariki leo Oktoba 31, 2021 akiwa jijini Dar es Salaam.

"Taarifa na taratibu za mazishi zitatolewa baadae,"ameeleza Makamu Mkuu wa chuo kupitia taarifa hiyo iliyoonwa na DIRAMAKINI BLOG hapa kama inavyosomeka hapa chini.

Post a Comment

0 Comments