Vijana waaswa kuenzi waasisi wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume

Na Mwandishi Wetu, CHATO

Vijana nchini waaswa kuenzi na kuishi fikra za waasisi wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume ili waweze kuwa wazalendo sambamba na kudumisha tunu za Taifa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameeleza hayo wakati wa ufunguzi wa Mdahalo wa Vijana Kitaifa uliofanyika katika Shule Sekondari Chato mkoani Geita tarehe 10 Oktoba, 2021.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wakati wa Mdahalo wa Vijana Kitaifa ikiwa ni moja ya shughuli katika kuelekea kilele cha siku ya Vijana , Mdahalo huo ulifanyika katika Shule ya Sekondari ya Chato Oktoba 10, 2021 mkoani Geita.

Waziri Mhagama alieleza kuwa tunazo sababu za msingi za kuwakumbuka waasisi wa taifa hili ambao ni Baba wa Taifa na mwasisi wa mapinduzi ya Zanzibar hasa kwa mchango wake mkubwa usio sahaulika kwa Taifa letu.

“Mchango huu wa waasisi wetu ni vyema urithishwe kwa vizazi vilivyopo hususan vijana na vizazi vijavyo ili waweze kuwa wazalendo kwa taifa lao na wakaziishi falsafa za viongozi hao,” alieleza Waziri Mhagama.

Aliongeza kuwa vijana wanapaswa kuendeleza mambo mema yote aliyoyafanya Baba wa Taifa enzi za uhai wake na Sheikh Abeid Aman Karume ili waendelee kujivunia juu ya misingi ya amani na umoja iliyopo nchini.

Aidha alifafanua kuwa, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kujenga umoja wa Kitaifa na kudumisha amani ya muda mrefu tuliyo nayo leo kama Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule akitoa salamu za Mkoa wakati wa Mdahalo wa Vijana Kitaifa ikiwa ni moja ya shughuli katika kuelekea siku ya Vijana Duniani , Mdahalo huo ulifanyika katika Shule ya Sekondari ya Chato hii leo Oktoba 10, 2021 mkoani Geita.

“Baba wa Taifa, aliasisi Mwenge wa Uhuru mwaka 1961 mara tu nchi yetu ilipopata Uhuru lengo lilikuwa ni kuutumia Mwenge wa Uhuru kama chombo cha kuhamasisha ujenzi wa Taifa lenye watu wenye amani, lenye watu wenye upendo, lenye watu wenye matumaini na lenye watu wenye heshima,” alisema

Pamoja na hayo alisisitiza vijana na wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuendeleza maono ya waasisi wa taifa na kuleta mageuzi ya kiuchumi yenye manufaa kwa taifa.

Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo pia kuwahimiza wananchi na wakazi wa Chato kushiriki kwenye Maonesho ya Wiki ya Vijana ambayo yanafanyika katika Viwanja vya Mazaina sambamba na kushiriki kwenye kilele cha Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika Uwanja wa Magufuli Chato Mkoani Geita tarehe 14 Oktoba, 2021.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fatma Hamad Rajab akieleza utekelezaji wa shughuli za Vijana Zanzibar wakati wa Mdahalo huo.
Baadhi ya washiriki wa Mdahalo wa Vijana Kitaifa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa mdahalo huo.
Naibu Katibu Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi akizungumza kuhusu utekelezaji wa shughuli za masuala ya vijana nchini wakati wa mdahalo huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, Naibu Waziri wake (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule (kushoto kwa waziri) na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fatma Hamad Rajab (wa kwanza kulia) wakicheza wimbo wenye ujumbe maalum wa pongezi za Serikali ya Awamu ya Sita wa kwaya ya Mwaganzega wakati wa mdahalo huo.
Kikundi cha burudani kikitumbuiza wakati wa mdahalo huo. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Rosemary Senyamule alisema kuwa ni vyema vijana wakatumia fursa ya mdahao huo ili waweze kutambua vyema historia ya Waasisi wa Taifa na kutambua maudhui ya Mwenge wa uhuru ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kuwaunganisha watanzania na kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii ili wajiletee maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa, Richard Jaba akitoa salamu wakati wa mdahalo huo alisema ni heshima kubwa kwa vijana kupata fursa za kujumuika pamoja na kueleza masuala yao huku akipongeza uamuzi ya kuleta shughuli hizo katika mkoa wa Geita na kuwaasa vijana kuendeleza umoja, mshikamano na upendo ili kuendelea chukangia katika kuleta maendeleo nchini.

“Kalenda ya chama inatambua uwepo wa wiki la vijana, hivyo tunaunga mkono kwa vitendo uwepo wa mdahalo huu na tutaendelea kutoa ushirikiano kwenu pia tunashukuru kuleta shughuli hizi Geita.,”alisema Jaba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news