Vilio vyatawala misa ya kuuaga mwili wa mwandishi Doris Ntaliaga Meghji

Na Dotto Mwaibale, Singida

SIMANZI, Vilio na Majonzi vilitawala katika Misa Takatifu ya kumuaga marehemu Mwanabahari Doris Meghji iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Jimbo la Singida.
Akiongoza misa hiyo, Askofu wa Jimbo Katoliki Singida, Mhashamu Edward Mapunda amesema, kanisa hilo limempoteza mwanahabari huyo ambaye alikuwa mtangazaji wa Radio Maria ambayo inasimamiwa na kanisa hilo.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mwanahabari Doris Ntaliaga wakati wakitoka katika Misa Takatifu ya kumuaga iliyofanyika Kanisa Katoliki Jimbo la Singida.
Marehemu Doris Ntaliaga Meghji enzi za uhai wake.
Askofu wa Jimbo Katoliki Singida, Mhashamu Edward Mapunda aliyeongoza Misa hiyo akiweka msalaba kwenye kaburi la marehemu Doris Meghji wakati wa maziko yake.
Mama wa marehemu Doris Meghji, Margareth Malecela akiwa na huzuni kwenye misa hiyo.

"Namfahamu Doris kama mlivyosikia yeye ndiye alikuwa mtangazaji wa kwanza wa Radio Maria tulipotangaza nafasi ya kazi Doris alijitokeza na kuwa mwakilishi wa Radio yetu ,”amesema Askofu Mapunda.

Mapunda amesema, walimkubalia kufanya kazi baada ya kujiridhisha kwamba alikuwa ni mwandishi wa habari mzuri na kuwa hata baada ya kupata nafasi hiyo alifanya kazi yake vizuri ya kutangaza neno la Mungu kupitia radio hiyo.

Alisema Doris alitangaza injili kupitia radio hiyo kwa kuwa alikuwa akihifahamu vizuri imani ya Kanisa Katoliki hivyo kutokana na kazi hiyo wanampongeza sana.

Alisema, Doris alimuaga kuwa amepata nafasi nyingine ya kazi TBC ambapo alimpa baraka zote ili apate nafasi nyingi zaidi za kulitumikia Taifa baada ya kupata uzoefu mkubwa katika Radio Maria.
Baba wa marehemu Doris, Mzee Meghji akiwa na huzuni kwenye misa hiyo.
Ni vilio na huzuni kwenye misa hiyo.
Misa ikiendelea.
Misa ikiendelea.
Ni huzuni kwenye misa hiyo. Hawa jamaa hawaamini kama mpendwa wao Doris amefariki na hawatamuona tena.
Utoaji sadaka ukifanyika.
Misa ikiendelea.
Zoezi la kuaga na kutoa heshima mbele ya mwili wa marehemu likifanyika.
Mama wa marehemu Doris Meghji, Margareth Malecela akimuaga mwanaye.

Alisema, anaamini na TBC aliwawakilisha vizuri kabla ya kupata nafasi nyingine ya kulitumikia Taifa kwa nafasi ya Afisa Tarafa mkoani Tanga ambayo aliifanya hadi umauti wake.

”Tuendelee kumuombea, kwani kifo cha Doris ni cha baraka, neema na ni mlango wa kuingia mbinguni.. kumuona Mungu,” alisema Askofu Mapunda.

Wakizungumza wakati waakitoa salamu za rambirambi katika Misa hiyo watu mbalimbali waliokuwa wakimfahamu Doris walisema alikuwa mchapa kazi na alimuheshimu kila mtu bila kujali jinsia yake, cheo chake na umri wake.

Walisema mkoani Tanga alikokuwa akifanya kazi alichaguliwa kuwa kiongozi wa maafisa tarafa wote wa mkoa huo, hivyo inaonesha ni jinsi gani alivyokuwa akishirikiana na wenzake vizuri katika kazi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Singida, Elisante John alisema chama hicho kimempoteza mwanahabari mahiri licha ya kuwa alikuwa akifanya kazi nyingine ya Afisa Tarafa.
Ni vilio na huzuni wakati wakitoka kwenye misa hiyo.
Mazishi yakifanyika.
Maafisa Tarafa kutoka Tanga, Singida na mikoa mingine wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la mwenzao Doris.
Baadhi ya Wanahabari wa Mkoa wa Singida wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la mwanahabari mwenzao Doris Meghji.

Baba na Mama wa marehemu wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa mtoto wao Doris Ntaliaga Meghji.

“Doris alikuwa mwenzetu na tulifanya naye kazi vizuri tukiwa wote hapa Singida na mimi ndiye niliyempokea na alikuwa mchapa kazi mzuri,”alisema John.

Marehemu Doris Meghji alizaliwa Septemba 15, 1977 mkoani Tabora wakiwa watoto wa kwanza na pacha wake Dorica Meghji ambaye naye ni marehemu.

Marehemu Doris alipata elimu ya Msingi Shule ya Msingi Utemini na baadae Shule ya Sekondari ya Margaret iliyopo mkoani Kilimanjaro.

Baada ya hapo marehemu alisoma kidato cha Tano na cha Sita Shule ya St.Joseph iliyopo Arusha na baada ya hapo alijiunga na Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) jijini Mwanza ambapo alisomea Uandishi wa Habari Ngazi ya Cheti na kuendelea na masomo zaidi ya fani hiyo hadi kupata Shahada.

Enzi za Uhai wake marehemu alifanya kazi sehemu tofauti tofauti kama Sibuka FM, EFM, Gazeti la Tanzania Daima, Mtangazaji wa Radio Maria, TBC, Standard FM, Azam TV na Afisa Tarafa Ngamiani mkoani Tanga.

Maziko ya Mwanahabari huyo yalihudhuriwa na viongozi kutoka Serikalini, vyama vya siasa, madiwani, Meya wa Manispaa ya Singida na wananchi kutoka sehemu mbalimbali wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Ramadhan Mussa Sima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news