Waganga wa tiba asili Gambosi wamuomba Askofu awaombee wapate mvua

Na Derick Milton, Simiyu

Waganga wa tiba asili katika kijiji na kata ya Gambosi Wilayani Bariadi Mkoa Simiyu, wamemuomba Askofu Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu awaombee ili mwaka huu waweze kupata mvua ya kutosha kwa ajili ya kilimo.

Mbali na ombi hilo, waganga hao wamemuomba Askofu huo kuwasaidia kuwajengea ofisi katika kijiji hicho ili waweze kuwa kutambilika rasmi na kazi zao waweze kuzifanya kwenye eneo moja alinalotambulika.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga, Mhashamu Liberatus Sangu pichani juu, akiwapatia redio ujumbe wa dini, waganga wa tiba ya asili katika kijiji cha Gamboshi wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu. 

Waganga hao wamewasilisha maombi hayo kwa Askofu huyo alipokutana nao jana kijijini kwa na kuzungumza nao mambo mbalimbali ikiwemo kudumisha mila na desturi za Kisukuma, kujikinga na Ugonjwa wa Uviko-19, kupiga vita ramli chonganishi.

Katika mkutano huo ambao ulifanyika kwenye viwanja vya kanisa Katiliki Kigango cha Gamboshi, waganga hao walimuomba Askofu huyo kutokana na kuelekea katika msimu wa kilimo awaombee wapate mvua ya kutosha.

“ Mwashamu Baba Askofu tunashukuru sana kukutana na sisi lakini kufika kijijini kwetu, hii ni neema kubwa sana, tunakuomba tunapoelekea msimu mpya wa kilimo utuombee kwenye kijiji chetu tuweze kupata mvua ya kutosha mwaka huu,” alisema Isabile Magaja.

Naye Mwenyekiti wa waganga hao Saguda Busaliguka alimuomba Askofu Sanga kuwasaidia waweze kupata ofisi kijijini hapo kwa ajili ya kufanyia kazi za kwa amani, huku akieleza uwepo wa amani na upendo katika kijiji hicho.

“Watu wamekuwa wakitambua Gamboshi kama kijiji cha uchawi Tanzania, lakini jambo hilo siyo kweli, hapa ni Amani na upendo, tunashukuru Askofu kwa kuja hapa kisha kukutana na sisi,” alisema Busaliguka.

Awali Mhashamu Askofu Liberatus Sangu, akizungumza katika mkutano huo, aliwataka waganga hao kuwa kielelezo kikubwa kwenye jamii katika kutunza na kuenzi mila na desturi za kisikuma.

“Kupitia kazi yenu mnayo nafasi kubwa kwenye jamii kuhimiza Mila na desturi kulinda, kupiga vita mambo maovu kama mauaji ya Albino, mauaji ya wazee na vikongwe, lakini pia kupiga vita utoaji wa mimba wanawake,” alisema Mhashamu Askofu Sangu.

“Mungu ametuumba binadamu wote sana, kuwaua albino, kutoa mimba ni kumkosea Mungu, nyie mnafanya kazi hizi kwa wema, mnatibu watu kwa miti shamba jambo jema hata kwa Mungu, lakini ni wajibu wetu kupiga vita matukio haya,” alisema Mhashamu Baba Askofu Sangu.

Katika hatua nyingine, Kiongozi huyo wa Dini aliwataka wananchi wa kijiji hicho pamoja na waganga wa tiba asili, kujenga utamaduni wa kupeleka watoto shule na siyo kuwafanyisha kazi za nyumbani.

Post a Comment

0 Comments