WATENDAJI TIMIZENI WAJIBU-NAIBU WAZIRI MARY MASANJA

Na Happiness Shayo- WMU

Watendaji wa Mikoa, Wilaya, Miji na Vijiji nchini wametakiwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kuhakikisha wanasimamia vizuri maeneo ya hifadhi ili kuepusha migogoro kati ya wananchi na Serikali.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) alipokuwa akizungumza na watendaji wa mkoa wa Singida katika kikao cha Mawaziri 8 chenye lengo la kutatua migogoro ya ardhi kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na watendaji wa Mkoa wa Singida wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Mawaziri 8 wa Kisekta yenye lengo la kutatua migogoro ya ardhi walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida leo.
Kamati ya Mawaziri 8 wa Kisekta ikiongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (Mb) (katikati) ikimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na watendaji wa Mkoa wa Singida leo.

“Migogoro ya wananchi kuvamia maeneo ya hifadhi inajitokeza wakati watendaji wenye dhamana na walioajiriwa na Serikali wapo wanatazama tu mpaka inafikia katika hali hii,” Mhe. Masanja amefafanua.

Mhe. Masanja ameongeza kuwa mtendaji yeyote atakayehusika katika kusababisha migogoro ya wananchi kwa kutosimamia vizuri eneo lake la kazi hastahili kwenda na kasi ya awamu ya sita na ana mpango wa kurudisha nyuma jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan za kutatua migogoro.
Baadhi ya watendaji kutoka katika Wizara mbalimbali za Kisekta wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na watendaji wa Mkoa wa Singida leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akitia saini kitabu cha wageni wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Mawaziri 8 wa Kisekta yenye lengo la kutatua migogoro ya ardhi walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida leo.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ludovick Nduhiye akifuatilia mada wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Mawaziri 8 wa Kisekta yenye lengo la kutatua migogoro ya ardhi walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida leo.

“Hakikisheni kwamba maeneo yote ya hifadhi ambayo tunayaachia kwa ajili ya wananchi mnayasimamia vizuri ili kumpa nafasi Mhe. Rais kutekeleza majukumu yake vizuri ya kuwahudumia wananchi.

Ameongeza kuwa migogoro hiyo ambayo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameisimamia na kutoa suluhu yake kwa kuiagiza Kamati ya Mawaziri 8 wa Kisekta kuitatua si vyema ikajirudia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news