Waziri Mkenda awapongeza Minjingu kwa kuzalisha mbolea ya tumbaku

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda, amepongeza uongozi wa kiwanda cha mbolea cha Minjingu kilichopo Kata ya Nkaiti wilayani Babati mkoani Manyara kwa kuanza kutengeneza mbolea ya zao la tumbaku.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Minjingu Mines Fertilizer Limited, Bw. Tosky Hans akimuonesha Waziri wa Kilimo Mhe. Profesa Adolf Mkenda aina mbalimbali za mbolea wakati alipokuwa akitembelea katika kiwanda hicho kilichopo Minjingu wilayani Babati mkoani Manyara leo Ijumaa Oktoba 8,2021.

Waziri Profesa Mkenda ameyasema hayo alipofanya ziara ya siku moja ya kukagua, kutembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu leo Oktoba 8, 2021.

Amesema, uongozi wa kiwanda cha Minjingu, umefanya jambo jema kwa kuzalisha mbolea mpya ya zao la tumbaku, ambayo itawanufaisha wakulima wa zao hilo.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Profesa Adolf Mkenda akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Minjingu Mines Fertilizer Limited, Bw. Tosky Hans mara baada ya kuwasili katika kiwanda hicho kilichopo Minjingu wilayani Babati mkoani Manyara leo Ijumaa Oktoba 8,2021 kwa lengo la kutembelea na kuona hali ya uzalishaji wa mbolea kiwandani hapo hasa kwa kipindi hiki ambacho tunaelekea katika msimu wa kilimo.
Waziri wa Kilimo Mhe. Profesa Adolf Mkenda akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi katika Kiwanda cha Minjingu Mines Fertilizer Limited, Bw. Tosky Hans mara baada ya kuwasili katika kiwanda hicho kilichopo Minjingu wilayani Babati mkoani Manyara leo Ijumaa Oktoba 8,2021 katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Minjingu Mines Firtlizer Limited, Bw. Tosky Hans.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Profesa Adolf Mkenda akimuonesha jambo Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Minjingu Mines Fertilizer Limited, Bw. Tosky Hans mara baada ya kuwasili katika kiwanda hicho kilichopo Minjingu wilayani Babati mkoani Manyara leo Ijumaa Oktoba 8,2021.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Profesa Adolf Mkenda na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Minjingu Mines Fertilizer Limited, Bw. Tosky Hans wakizungumza mara baada ya kuwasili katika kiwanda hicho kilichopo Minjingu wilayani Babati mkoani Manyara leo Ijumaa Oktoba 8,2021.

Amesema, ni vyema mbolea ya zao la tumbaku kuzalishwa nchini kwani ajira za watanzania zitapatikana na kuokoa fedha za kigeni kwa kuagiza nje ya nchi.

Hata hivyo, Waziri Mkenda ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kufanya kazi mchana na usiku ili kuzalisha kiasi kikubwa cha mbolea.

Amesema, endapo kiwanda hicho kikifanya kazi mchana na usiku, uzalishaji wa mbolea utakuwa mkubwa hivyo kuwanufaisha wakulima nchini kutokana na mahitaji yake.

"Mahitaji ya mbolea ni makubwa nchini hivyo tekelezeni hilo kwani hata soko la walaji ni kubwa kutokana na wakulima nchini kuitumia mbolea," amesema Waziri Profesa Mkenda. Waziri wa Kilimo, Mhe. Profesa Adolf Mkenda akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Minjingu Mines Fertilizer Limited, Bw. Tosky Hans alipokuwa akimuonesha bei mbalimbali za mbolea katika kipeperushi wakati akitembelea katika kiwanda hicho kilichopo Minjingu wilayani Babati mkoani Manyara leo Ijumaa Oktoba 8,2021.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Profesa Adolf Mkenda akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Minjingu Mines Fertilizer Limited, Bw. Tosky Hans alipokagua mgodi unaochimbwa madini ya kutengenezea mbolea.
Moja ya migodi inayochimbwa madini ya kutengenezea mbolea katika kiwanda cha mbolea cha Minjingu Mines Fertilizer Limited.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Minjingu Mines Fertilizer Limited, Bw. Tosky Hans akimuonesha Waziri wa Kilimo Mhe. Profesa Adolf Mkenda maeneo mbalimbali yanayochimbwa madini ya kutengenezea mbolea wakati akitembelea katika kiwanda hicho kilichopo Minjingu Wilayani Babati Mkoani Manyara leo Ijumaa Oktoba 8,2021.
Baadhi ya wataalam wa kiwanda hicho wakipima udongo kwa ajili ya kutengenezea mbolea.

Amesema, mbolea hizo zinaweza kuhifadhiwa kwenye maghala ya serikali wakati wa usambazaji na kiwanda hicho kikachangia gharama kwa kulipia kiasi cha fedha.

Mkurugenzi wa kiwanda cha mbolea cha Minjingu, Tosky Hans amesema watatekeleza agizo hilo la serikali na kuuza mfuko mmoja wa mbolea kilo 50 kwa shilingi 55,000.Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Minjingu Mines Fertlizer Limited Bw. Tosky Hans akimuonesha Waziri wa Kilimo Mhe. Profesa Adolf Mkenda maeneo ya kiwanda hicho kilichopo Minjingu Wilayani Babati Mkoani Manyara leo Ijumaa Oktoba 8,2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Minjingu Mines Fertlizer Limited, Bw. Tosky Hans akimpitisha Waziri wa Kilimo Mhe. Profesa Adolf Mkenda maeneo mbalimbali wakati akitembelea katika kiwanda hicho kilichopo Minjingu wilayani Babati mkoani Manyara leo Ijumaa Oktoba 8,2021.
Muonekano wa baadhi ya maeneo ya kiwanda hicho.

Hans amesema, hata mbolea ya Minjingu ikisafirishwa kwenda maeneo mbalimbali nchini hawatazidisha bei ya shilingi 65,000.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania, Stephan Ngailo amesema mahitaji ya mbolea nchini ni tani 700,000 kwa mwaka hasa katika mikoa inayolima tumbaku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news