WAZIRI MWAMBE AKAGUA UWEKEZAJI WA KIWANDA KIPYA CHA MBOLEA DODOMA

NA MWANDISHI MAALUM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji , Mhe. Geoffrey Mwambe, leo tarehe 16 Oktoba, 2021, amekagua shughuli za uwekezaji katika Mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha kuzalisha Mbolea asilia cha ITRACOM FERTILIZERS LIMITED, kinachojengwa katika eneo la Nala, jijini Dodoma.
Mradi huo ni miongoni mwa miradi yenye hadhi ya uwekezaji maaluum, ukiwa na mtaji wa Dola za Marekani milioni 180 na unatarajiwa kuzalisha ajira 3000. Aidha, mradi huo utasaidia kuingiza fedha za kigeni, kipato kwa wananchi na mapato ya serikali kupitia kodi.

Katika ziara hiyo Mhe. Mwambe ameabatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka pamoja na Watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news