Waziri wa Nishati afanya mazungumzo na Balozi wa Marekani na Uholanzi, ataja vipaumbele

Na Theresia Mhagama-WN

Waziri wa Nishati, January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald J.Wright pamoja na Balozi wa Uholanzi, Wiebe De Boer ambapo alitaja vipaumbele katika Sekta ya Nishati.
Waziri wa Nishati, January Makamba (kulia) akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Donald J. Wright katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati mkoani Dar es Salaam tarehe 08 Oktoba, 2021. Mazungumzo yao yalihusu masuala mbalimbali kuhusu Sekta ya Nishati.

Mazungumzo yake na Mabalozi hao yalifanyika tarehe 8 Oktoba, 2021 katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati zilizopo mkoani Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watendaji mbalimbali akiwemo Kamishna wa Umeme na Nishati na Jadidifu, Felchesmi Mramba, Kamishna wa Petroli na Gesi, Michael Mjinja, na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio.

Katika kikao chake na Balozi wa Marekani, Waziri Makamba alimueleza Balozi huyo vipaumbele mbalimbali vya Serikali katika Sekta ya Nishati ikiwemo upatikanaji wa umeme hasa katika maeneo ya vijijini, kwani Serikali imefanya kazi kubwa ya kupeleka umeme maeneo hayo lakini wananchi wengi bado wanahitaji huduma hiyo.
Afisa Biashara Mwandamizi katika Ubalozi wa Marekani, Ken Walsh (kushoto) akizungumza jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Nishati, January Makamba (kulia) na Balozi wa Marekani nchini, Donald J.Wright kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati mkoani Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati, January Makamba (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Marekani nchini, Donald J.Wright mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati mkoani Dar es Salaam tarehe 08 Oktoba, 2021.
Waziri wa Nishati, January Makamba (Wa Tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Marekani nchini, Donald J.Wright (wa Nne kushoto) mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati mkoani Dar es Salaam tarehe 08 Oktoba, 2021. Wengine katika picha ni Watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Ubalozi wa Marekani.

Alitaja kipaumbele kingine kuwa ni uwepo wa nishati endelevu za kupikia mfano gesi ya kwenye mitungi (LPG) ambayo itawafanya wananchi wengi waache kutumia mkaa na kuni kwa kupikia na hivyo kuondoa suala la uharibifu wa misitu ambalo pia linapelekea mabadiliko ya tabia nchi.

“Kipaumbele kingine, ni kuzifanya Taasisi zilizo chini ya Wizara kama vile TANESCO, TPDC na EWURA, kuwa na uwezo wa RasiliMali Watu pamoja na uwezo wa kifedha utakaoziwezesha Taasisi hizo kuwa na ufanisi pamoja na usimamizi madhubuti wa Sekta ya Nishati hasa katika kipindi ambacho Tanzania inaenda kuwa nchi yenye umeme wa kutosha katika ukanda huu,"alisema Makamba.

Kwa upande wake Balozi wa Marekani, Donald J. Wright, alisema ataendelea kufanya kazi na Wizara na kwamba kumekuwa na ushirikiano wa takriban miaka 60 kati ya Tanzania na nchi hiyo na eneo mojawapo la ushirikiano huo ni sekta ya Nishati.
Waziri wa Nishati, January Makamba (kulia) akizungumza na Balozi wa Uholanzi nchini, Wiebe De Boer katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati mkoani Dar es Salaam tarehe 08 Oktoba, 2021. Mazungumzo yao yalihusu masuala mbalimbali kuhusu Sekta ya Nishati.

Katika mazungumzo yake na Balozi wa Uholanzi nchini, Wiebe De Boer, Waziri wa Nishati alitaja maeneo mbalimbali yanayohitaji ushirikiano, kubwa ikiwa ni kupeleka umeme katika maeneo ambayo hayajafikiwa na umeme wa gridi kama vile visiwa kwa kuweka mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali ikiwemo Jua ambalo linapatikana katika maeneo yote ya Tanzania.
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Wiebe De Boer (kushoto), akizungumza na Waziri wa Nishati, January Makamba katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati mkoani Dar es Salaam tarehe 08 Oktoba, 2021. Mazungumzo ya viongozi hao yalihusu masuala mbalimbali kuhusu Sekta ya Nishati.

Aliishukuru Uholanzi kwa kuwa na ushirikiano mzuri na Tanzania kwa miaka mingi na kwamba ushirikiano wa nchi hizo mbili upo katika sekta mbalimbali ikiwemo nishati.
Waziri wa Nishati, January Makamba (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini, Wiebe De Boer mara baada ya kumaliza mazungumzo kuhusu Sekta ya Nishati nchini. Kikao kilifanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati mkoani Dar es Salaam tarehe 08 Oktoba, 2021.

Balozi wa Uholanzi, Wiebe De Boer alimweleza Waziri wa Nishati kuwa, Serikali isisite kuwasiliana na Ubalozi huo pale inapoona kuna uhitaji wa kuungwa mkono mkono katika utekelezaji wa mipango mbalimbali.
Waziri wa Nishati, January Makamba (Wa Nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini, Wiebe De Boer (wa Nne kushoto) pamoja na viongozi kutoka Wizara ya Nishati na baadhi ya Taasisi zilizo chini ya Wizara mara baada ya kumalizika kwa kikao baina yao kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati mkoani Dar es Salaam tarehe 08 Oktoba, 2021.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news