Waziri wa Nishati, Naibu Waziri wakagua Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP)

Na Theresia Mhagama-WN

Waziri wa Nishati, January Makamba pamoja na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato wamekagua kazi mbalimbali zinazoendelea kutekelezwa katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere unaotekelezwa wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani.
Waziri wa Nishati, January Makamba ( aliyenyoosha mkono), akizungumza jambo katika eneo inapojengwa mitambo ya kuzalisha umeme katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato.
Waziri wa Nishati, January Makamba ( Wa Tatu kulia), akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato ( Wa Tano kushoto) mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja la kudumu katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere. Wa Saba kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato. Wa Nane kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali.
Waziri wa Nishati, January Makamba ( Wa Pili kushoto), akiangalia kazi mbalimbali zinazoendelea kufanyika katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere. Wa kwanza kushoto ni Mhandisi Mkazi wa Mradi, John Mageni.
Waziri wa Nishati, January Makamba ( Wa kwanza kushoto), na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato ( Wa Pili kushoto) wakiangalia mchoro unaohusu mashine za kufulia umeme (turbines) katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere. Wa kwanza kulia ni Mhandisi Mkazi wa Mradi wa Julius Nyerere, John Mageni.
Waziri wa Nishati, January Makamba ( Wa Nane kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na TANESCO mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja la kudumu katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere. Wa Saba kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato. Wa Nane kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali.

Ukaguzi huo umefanyika kabla ya ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Philip Isdor Mpango katika mradi huo itakayofanyika tarehe 12 Oktoba, 2021.

Katika ukaguzi huo, viongozi hao waliambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Felchesmi Mramba, Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme, Mhandisi Styden Rwebangila na watendaji wengine kutoka Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) na kutoka mradi wa umeme wa Julius Nyerere ( JNHPP).

Maeneo waliyokagua ni pamoja Tuta Kuu la Bwawa, Njia za kupeleka maji kwenye mitambo ya kuzalisha umeme, Jengo la mitambo pamoja, kituo cha kupokea na kusafirisha umeme pamoja na ujenzi wa daraja la kudumu.

Post a Comment

0 Comments