Wizara ya Kilimo:Tuna wajibu wa kuwalinda wakulima wote

NA MWANDISHI MAALUM

SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imesema ina wajibu wa kuwalinda wakulima nchini kwa namna yoyote ile.

Akiwa katika ziara mkoani Katavi, Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema hayo kufuatia taarifa ya Wilaya ya Tanganyika iliyolalamikia Mamlaka ya Wanyama Pori (TAWA) kuweka alama za mipaka katika misitu ya Tongwe.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akiongozana na Kaimu Meneja wa TFRA Sumbawanga na Mpanda, Bw. Range Marwa, Mbunge wa Jimbo la Kwera, Mhe. Deus Sangu anayeongea na simu pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali katika ukaguzi wa zoezi la ununuzi wa mahindi kupitia NFRA wilayani Sumbawanga. (Picha na Wizara ya Kilimo).

Misitu ya Tongwe iliyopo wilayani Tangayika imekuwa ikisimamiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ambapo miezi michache iliyopita ilipokea tangazo la serikali linaloeleza misitu hiyo kuwa chini ya usimamizi wa TAWA bila kushirikishwa

Aidha,katika misitu hiyo wilaya imetenga maeneo ya uwekezaji likiwemo kilimo.Naibu Waziri Bashe ameitaka wilaya hiyo kutowatoa wakulima wote ambao tayari wamekwishagawiwa maeneo ya uwekezaji katika kilimo.

"Haiwezekani TAWA kutumia vibaya mamlaka waliyinayo, waliwezaje kuingia na kuweka bikoni bila kushirikisha uongozi wa vijiji, kata au wilaya,"amesema.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga na Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA, Milton Lupa, Mbunge wa Jimbo la Kwera Mhe. Deus Sangu na viongozi mbalimbali wa Serikali katika ukaguzi wa zoezi la ununuzi wa mahindi kupitia NFRA wilayani Sumbawanga. Naibu Waziri wa Kilimo  Mhe. Hussein Bashe akisikiliza maelezo ya Mwenyekiti wa Chama Kikuu Cha Ushirika cha Ufipa, Bw. Adabeth Mbuyani kuacha kukopa fedha taslimu kwa mabenki kwa ajili ya kununulia mbolea wakati alipokagua ununuzi wa mahindi katika kituo cha Sumbawanga mkoani Rukwa akiwa kwenye ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe akitoa maagizo kwa Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ufipa Bw. Adabeth Mbuyani kuacha kukopa fedha taslimu kwa mabenki kwa ajili ya kununulia mbolea wakati alipokagua ununuzi wa mahindi katika kituo cha Sumbawanga mkoani Rukwa akiwa kwenye ziara ya kikazi.
Wakulima akina mama wakichambua mahindi yao tayari kuyauza kwa NFRA ghala la mahindi TFC Sumbawanga alipokuwa katika ziaya ya kikazi kukagua zoezi la ununuzi wa mahindi unaofanywa na serikali kupitia NFRA.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akitoa maelekezo kwa wakulima wanaochambua mahindi yao tayari kuyauza kwa NFRA ghala la mahindi TCF Sumbawanga alipokuwa katika ziaya ya kikazi kukagua zoezi la ununuzi wa mahindi unaofanywa na serikali kupitia NFRA.
Baadhi ya vibarua wakipakia mahindi kwenye gari katika ghala la TFC Laela ambapo NFRA imeweka kituo cha kununulia mahindi.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akizungumza na wauzaji wa mahindi wakati alipokagua ununuaji wa mahindi katika kituo cha NFRA Laela.
Baadhi ya akina mama wakichambua mahindi katika kituo cha kununulia mahindi cha Laela mkoani Rukwa.

Bashe ameeleza kuwa, kitendo hicho ni sawa na kumchonganisha Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi wake.

Ameongeza kuwa, suala hilo linahitaji mashauriano zaidi baina ya Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mali Asili na Utalii hivyo kukataza halmashauri kutowaondoa wananchi waliopo katika maeneo hayo

Aidha, ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika kutenga eneo la ekari 1000 kwa ajili ya kilimo cha mbegu kufuatia mkoa wa Katavi kuwa kitovu cha uzalishaji wa mbegu ambapo watafiti wa Taasisi za TARI na ASA watashughulikia uzalishaji huo wa mbegu.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akiangalia ubora wa mahindi wakati alipokagua kituo cha kununulia mahindi cha Sumbawanga.
Mahindi yakiwa yamehifadhiwa katika ghala la TFC kituo cha kununulia mahindi cha NFRA Sumbawanga mjini.

Naibu Waziri Bashe alisisitiza umuhimu wa viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya kata, halmashauri na wilaya kuhakikisha wanalinda ardhi ya wakulima, kwa kutenga na kupima ardhi ya kilimo, kama ilivyo katika ardhi ya hifadhi, vyanzo vya maji au hifadhi za taifa.

"Kwa kuwa watu wanazidi kuongezeka lakini ardhi haingozeki, hivyo mahitaji ya ardhi ya kulima inaongezeka, ni muhimu sasa kwa halmashauri zetu kutenga na kupima ardhi ya kulimo, kuepusha migogoro inayoweza kutokea baadae, kama inavyohifadhiwa ardhi ya vyanzo vya maji, hifadhi ya misitu au mapori ya akiba, vivyo hivyo ardhi ya kilimo ihifadhiwe," alisema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news