Bruno Fernandes afunguka kuhusu kipigo cha Man United

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Erick Bailly aliyejifunga dakika ya saba na Bernardo Silva dakika ya 45 wameipa Manchester City ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji Manchester United.

Ni katika mtanange uliopigwa Novemba 6, 2021 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford.

Kwa matokeo hayo, Man City inafikisha alama 23 na sasa inazidiwa alama tatu na vinara, Chelsea wakati Man United inabaki na alama zake 17 baada ya timu zote mechi 11.

Akizungumzia matokeo hayo,kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Bruno Fernandes amesema kuwa, wachezaji wa timu hiyo wanatakiwa kujitazama upya ili kuboresha viwango vyao ili kuisaidia timu kushinda.

“Tunatakiwa kusema kidogo na vitendo vyetu kujieleza zaidi. Nazungumza ambayo tayari yamesemwa, tunatakiwa kubadilika sana, maana tumepoteza zaidi ya moja tena vibaya.Tukitaka kuwa kama wao inatakiwa tufanye zadi yao,"amesema Fernandes nyota huyo wa zamani wa Sporting Lisbon.

Awali, kikosi cha kocha Pep Guardiola kilitawala vyema mtanange huo kwa zaidi ya asilimia 68, huku wachezaji wa City wakiwa wamekimbia eneo kubwa la uwanja tofauti na United ambayo ilikuwa inaongozwa ikionyesha wazi udhaifu.
 (Picha na Getty Images).

Post a Comment

0 Comments