Fahamu zaidi kuhusu Shule ya Msingi Museveni mjini Chato

NA NTEGHENJWA HOSSEAH, Chato

SHULE ya Msingi Museveni iliyopo wilayani Chato mkoani Geita imejengwa kwa ufadhili wa Mhe. Yoweri Kaguta Mseveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda na itachukua wanafunzi wa Elimu ya Awali na Darasa la kwanza hadi la Saba.

Shule hii imesajiliwa kama shule ya kutwa na inatarajia kuwa itatumia mtaala wa Kiingereza (English Medium).
Majengo yaliyojengwa na kukamilika ni katika shule hii ni Jengo la Utawala 1, Vyumba vya madarasa ya Shule ya Msingi 17, Maktaba (Resource Centre) 1, Vyumba vya madarasa ya Elimu ya Awali 3, Ofisi kwa ajili ya Elimu ya Awali 2, Matundu ya vyoo 37 na Nyumba ya walimu (2 in 1).

Post a Comment

0 Comments