Hospitali ya Mandewa yakabidhiwa basi la kusafirishia wafanyakazi


NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKUU wa Mkoa wa Singida, Dkt. Binilith Mahenge leo Novemba 30, 2021 amezindua rasmi na kukabidhi basi aina ya Coasta kwa ajili ya kusafirishia wafanyakazi wa Hospitali ya Mandewa iliyopo mkoani hapo kama kitendea kazi kitakachowasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.
Akiongea na wafanyakazi akiwa hospitalini hapo baada ya kuwakabidhi basi Mkuu wa Mkoa amewapongeza watumishi kwa namna ambavyo wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu na wengi wao wakitumia bodaboda kufika kazini, lakini pia hawakukata tamaa.

RC Mahenge amemtaka Afisa Usafirishaji wa Hospitali ya Mkoa wa Singida kuhakikisha kwamba basi hilo linatunzwa na kuzingatia muda wa kufanyia huduma (service) kila inapofika muda wake ili kulifanya lidumu kwa muda mrefu na kuendelea kuwasaidia watumishi.
Amewataka madaktari katika hospitahi hiyo ambayo ni Tawi la Hospitali ya Mkoa wa Singida kuboresha huduma zao na kuzifanya ziwe za kibingwa ili kuifanya Singida kuwa kimbilio la mikoa ya jirani (center of excellence ).

Aidha, ameitaka bodi ya hospitali hiyo kuanza kufikiria namna ya kujenga nyumba za watumishi kupitia vyanzo vyao vya ndani au kupitia mashirika mbalimbali kwa kuwa kukaa karibu na hospitali kunaongeza ufanisi katika kazi.
Akimalizia hotuba yake mkuu wa mkoa amewataka madaktari hao pamoja na bodi kuyafanya majengo ya zamani kuwa hospitali ya wilaya halafu majengo ya Hospitali ya Mandewa yatumike kama hospitali ya mkoa.

Awali Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa, Dkt. Deogratius Banuba akisoma hotuba yake amesema gari hilo lina thamani ya zaidi ya sh. Milioni 236 ambazo zilitokana na makusanyo ya ndani.
Hata hivyo amemhakikishi RC kwamba gari hilo litatumika kubeba watumishi kuwaleta kazini na kuwarudisha na pia kutumika katika shughuli za kijamii kwa watumishi hasa zile ambazo zipo kisheria kama msiba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news