Jiandaeni kuwapokea Wahandisi 260 walioajiriwa hivi karibuni-Prof.Shemdoe

NA NTEGHENJWA HOSSEAH-OR TAMISEMI

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe amewaagiza Makatibu Tawala Mikoa, Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mameneja TARURA kuandaa mazingira bora kwa ajili ya kuwapokea wahandisi 260 walioajiriwa hivi karibuni.
Prof. Shemdoe ameyasema hayo alipokua ziarani Wilayani Chato kukagua miradi ya maendeleo hususani ujenzi wa madarasa kwa ajili ya kupokea kidato cha kwanza 2022 unaoendelea nchi nzima.

"Kulikua na changamoto ya kuchelewa kukamilika kwa miradi kwa sababu ya upungufu wa Wahandisi kwenye Mikoa na Halmashauri zetu hili tuliliona na tukachukia hatua za makusudi ili kuhakikisha kiwa hakuna mradi unaokwama kwa sababu hii,"amesema Prof. Shemdoe.
Ujenzi wa madara ukiendelea.
Amesema, Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imekamilisha zoezi la Ajira za Wahandisi kwa ajili ya Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).
"Jumla ya Wahandisi 260 wameajiriwa huku 14 wakipelekwa TARURA, 56 kwenye Sekretarieti za Mikoa na 190 kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

"Wahandisi hawa sasa wameshapangiwa vituo hivyo muwaandalie mazingira bora ya kuwapokea na kushughulikia stahiki zao mapema ili wafurahie kazi yao,"alisisitiza Prof. Shemdoe.

Post a Comment

0 Comments