Mahabusu wengine watoboa shimo kwenye ukuta wa sero na kutoroka nchini Kenya

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MAHABUSU Shadrack Leparan (29), Enoc Ndege (28) na Patrick Mausa (32) wametoroka kwenye kituo cha Polisi walikokuwa wakishikiliwa usiku wa kuamkia Jumamosi ya Novemba 20,2021 huko Narok nchini Kenya baada ya kufanikiwa kutoboa shimo kwenye ukuta wa sero ambayo walikuwa wamewekwa.

Polisi watatu ambao ni Carmax Okelo, Andrew Bett na Jalus Okoa watahojiwa kueleza jinsi mahabusu hao watatu walifanikiwa kutoroka wakati walikuwa wameshika doria.

Maafisa hao ambao walikuwa zamu usiku huo wamekamatwa kutokana na uzembe waliofanya mpaka mahabusu hao watatu kutoroka siku mbili kabla ya tarehe yao ya kufikishwa mahakamani.

Mahabusu hao waliotoroka usiku wa ni watuhumiwa wa mauaji na wizi walichimba shimo na kutoa matofali yaliyokuwa pembeni ya mlango wa sero na kutoroka, mahabusu wengine wawili waliobaki sero wanasema hawafahamu wenzao walivyotoroka saa ngapi.

Tukio hili limetokea siku tatu tu baada ya kukamatwa kwa washukiwa wa ugaidi ambao walitoroka kwenye jela ya Kamiti Jumapili iliyopita ambapo walikamatwa wakiwa safarini kuelekea Somalia.

Wafungwa hao watatu wanaohusishwa na visa vya ugaidi ambao walitoroka jela ya Kamiti nchini Kenya ni Musharaf Abdalla maarufu Alex Shikanda , Joseph Ouma na Mohammed Ali Abikar ambao walikamatwa katika eneo la Kitui Kusini mwa Kenya.

Watatu hao waliibua taharuki nchini Kenya walipotoroka kutoka jela yenye ulinzi mkali zaidi baada kutoboa ukuta wa jela hiyo.

Walitumia nguo blanketi na waya kutengeneza kamba ambazo walitumia kupanda kuta mbili ndefu za jela hiyo.

Kitendo hicho kilisababisha maafisa saba wa jela ya Kamiti kukamatwa kwa madai ya utepetevu uliowasaidia wahalifu hao kutoroka.

Awali Rais Uhuru Kenyatta alimwaamrisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Fred Matiangi kuhakikisha wanatumia kila mbinu kuwakamata wahalifu hao ambao alisema ni hatari kwa usalama wa Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news