Mheshimiwa Mary Masanja ahimiza Balozi kutangaza utalii wa Tanzania

NA HAPPINESS SHAYO-WMU

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amezihimiza balozi za Tanzania nchi mbalimbali kushirikiana na Wizara yake katika kutangaza vivutio vya utalii.
Balozi wa Tanzania Kigali-Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Richard Makanzo akimkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja alipotembelea Ofisi za Ubalozi mapema leo. Mhe. Masanja yupo nchini Rwanda kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Uongozi wa Utalii Afrika na Tuzo za Wiki ya Kusafiri litakalofanyika kesho kwenye hoteli ya Kigali Serena.

Ameyasema hayo leo kwenye kikao na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Richard Makanzo alipotembelea ubalozi huo.

Mhe. Masanja amesema kupitia balozi za Tanzania, utalii unaweza kukua kwa kiasi kikubwa.

“Mkishiriki katika matukio mbalimbali hapa nchini Rwanda na kutumia vipeperushi na majarida kuutangaza utalii wetu, idadi ya watalii itaongezeka,” amesisitiza Mhe. Masanja.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akisalimiana na watumishi wa ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda alipotembelea Ofisi za Ubalozi mapema leo. Mhe. Masanja yupo nchini Rwanda kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Uongozi wa Utalii Afrika na Tuzo za Wiki ya Kusafiri litakalofanyika kesho kwenye hoteli ya Kigali Serena.
Balozi wa Tanzania Kigali-Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Richard Makanzo (kulia) akichangia mada kuhusu mikakati ya kukuza utalii wa Tanzania alipotembelewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) ofisini kwake leo. Wengine ni Mkuu wa Fedha na Utawala, Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda, Happiness Ruangisa (wa pili kutoka kulia) na Mwambata wa Jeshi, Kanali Ramadhan Dogoli (wa tatu kutoka kulia)wakifuatilia mada.

Aidha, Mhe. Masanja ameutaka ubalozi huo kujenga mahusiano mazuri na wafanyabiashara wa sekta ya utalii na wawekezaji nchini Rwanda ili wavutiwe kuwekeza nchini Tanzania hasa katika maeneo ya fukwe na hifadhi ili kuiendeleza sekta hiyo.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Richard Makanzo amesema ofisi yake iko tayari kutoa ushirikiano kuhakikisha utalii wa Tanzania unakua.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utalii, Philip Chitaunga ameahidi kutoa ushirikiano kwa balozi za Tanzania za nchi mbalimbali ili kukuza utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akitoa maelekezo ya namna ya kukuza utalii kupitia balozi za Tanzania, alipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda mapema leo. Wengine ni Balozi wa Tanzania Kigali-Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Richard Makanzo (kulia), Mkuu wa Fedha na Utawala, Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda, Happiness Ruangisa (wa pili kutoka kulia) na Mwambata wa Jeshi, Kanali Ramadhan Dogoli (wa tatu kutoka kulia) wakifuatilia mada.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Philip Chitaunga (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu maboresho yaliyofanyika ya kuendeleza utalii nchini Tanzania wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (hayupo pichani) na Balozi wa Tanzania Kigali-Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Richard Makanzo (hayupo pichani).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na watumishi wa ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda mara baada ya kikao kilichofanyika mapema leo. Wengine ni Balozi wa Tanzania Kigali-Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Richard Makanzo (wa nne kutoka kulia) na Mkurugenzi Idara ya Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Philip Chitaunga (wa pili kutoka kushoto).

“Nitashirikiana na balozi kwa kuhakikisha vipeperushi, majarida, video na taarifa zozote zinazoongelea utalii wa Tanzania zinapatikana kwa urahisi” Bw. Chitaunga amesisitiza.

Amesema kuwa ni muhimu ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuwezesha watalii wanaokuja Rwanda waweze kutembelea Tanzania bila vikwazo.

Mhe. Mary Masanja yupo nchini Rwanda kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Uongozi wa Utalii Afrika na Tuzo za Wiki ya Kusafiri litakalofanyika kesho kwenye hoteli ya Kigali Serena.

Post a Comment

0 Comments