Miriam Odemba awapa faraja watoto wanaoishi mazingira magumu

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kuwasaidia watoto wenye mahitaji maamlumu wakiwemo yatima na wasiokuwa na walezi ili waweze kupata baraka zaidi katika maisha yao ya kila siku.
Mwanamitindo maarufu hapa nchini, Bi.Miriam Odemba ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji wa msaada wa vitu mbalimbali uliombatana na kupata chakula cha pamoja na watoto wenye mahitaji maalum wa Kituo cha Jeshi la Wokovu (Salvation Army) kilichopo Halmashauri ya Manispaa Temeke.

Amesema kuwa, Watanzania wamekuwa nyuma kwenye masuala ya kusaidia jamii, lakini kwenye shughuli za kuchangia harusi na sherehe mbalimbali wamekuwa wakijitokeza jambo ambalo wakati mwingine halina tija kwa jamii.

Pia amewataka warembo na wanamitindo wengine kuungana naye kuwawezesha wenye mahitaji maalum ili kuweza kutokomeza umasikini unaowasumbua watoto hao katika maeneo mbalimbali nchini.
Odemba amewaomba wafadhili wengine nchini na nje ya nchi kujitokeza kuwaunga mkono taasisi yake kwa kuwapa masaada ili kuendelea kusaidia watu wenye mahitaji maalum.

Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa kituo cha Salvation Army ,Bw. George Mbegani Mwasenga amesema kuwa, ujio wa Yaasisi ya Miriam Odemba imekuwa faraja kubwa kwa watoto hao wenye mahitaji maalum na kuwaomba watanzania wengine kujitokeza kwenda kuwatazama.
Aidha amesema kuwa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kuwama kwa baadhi ya mambo ambayo ni mahitaji maalum kwa watoto hao kutokana na gharama kuwa kubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news