Rais Dkt.Mwinyi: Tunapaswa kuyafanya mambo haya ili yajayo yafurahishe zaidi kiuchumi

NA MWANDISHI MAALUM

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema ili Taifa liweze kufanikisha matarajio ya kukuza Uchumi katika mwaka wa Pili wa Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nane, halina budi kuendelea kudumisha amani, uwajibikaji pamoja na watendaji kujenga uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Dkt. Mwinyi ametoa rai hiyo katika hotuba aliyotoa kwa wananchi katika kilele cha maadhimisho ya kutimiza mwaka mmoja wa Uongozi wake, hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip iliopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.

Amesema, katika mwaka wa Pili wa Uongozi wa Awamu ya Nane, Serikali imekopa jumla ya Shilingi Bilioni 460 kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) ambazo shiligni Bilioni 230 kati ya fedha hizo zitatumika kufanikisha miradi katika sekta mbali mbali za kijamii, ikiwemo Afya, elimu, maji safi na salama na umeme pamoja na kuwawe zesha wananchi kiuchumi.

Amesema, Shilingi Bilioni 230 zilizobaki zitatumika kwa ajili ya kulipia madeni ya Wazabuni, kulipa fidia mbali mbali pamoja na kulipia haki mbali mbali za wafanyakazi.

Amesema, fedha hizo (bilioni 230) zitakazoingizwa katika shughuli za kiuchumi ni nyingi sana na ni wazi kuwa zitaleta faida kubwa kwa Taifa pamoja na kurahisha maisha kutokana na mzunguko wa fedha.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Wananchi wa Zanzibar katika mkutano wake wa kuadhimisha Mwaka mmoja wa Uongozi wake, mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip Zanzibar.
Wananchi wakimshangilia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akiwahutubia Wananchi katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Uongozi wake.
Wananchi na wageni waalikwa wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayuypo pichani) akihutubia katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tuliup Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaniu Karume Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto kwake) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na (kulia kwake) Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Dkt.Amani Karume, alipowasili katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kuwahutubia Wananchi katika hafla ya kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Uongozi wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, alipowasili katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kuwahutubia Wananchi katika hafla ya kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Uongizi wake.(Picha na Ikulu).

Hivyo, alisema matarajio hayo yatakamilika tu endapo wananchi wataendelea kudumisha amani iliopo, sambamba na watendaji kuanzia ngazi za chini za uongozi kuwajibika ipasavyo na kufanya kazi zao kwa uadilifu, hususan katika suala la tenda.

Alieleza kuwa katika kipindi kilichopita miradi mingi ilishindwa kukamilishwa vyema kwa sababu ya Rushwa na kubainisha viashiria vilivyoanza kujichomoza na kusisitiza kwamba yeyote atakaejaribu kuchota fedha hizo hatomuachia.

Rais Dkt.Mwinyi alitoa indhari juu ya matumizi stahiki ya fedha hizo, huku akiahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria watendaji wote watakaojihusisha na udokozi au upotevu wa fedha hizo.

Katika hatua nyengine, Dkt. Mwinyi alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa alizochukua kufanikisha kupatikana kwa mkopo huo pamoja na ukaribu wake kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao umekuwa chachu ya kuondokana na changamoto mbali mbali zinazojitokeza.

Aidha, Dkt. Mwinyi alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanya uamuzi wa kuwalipa fedha zao (kiasi cha Shilingi Bilioni 38.7) wahanga wote wa iliokuwa Masterlife, ikiwa ni hatua ya kuwaondolea usumbufu wa maisha wananchi masikini walioweka fedha hizo

Post a Comment

0 Comments