Rais Samia ahudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanaoshiriki COP 26

NA MWANDISHI MAALUM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 1 Novemba, 2021 amehudhuria ufunguzi rasmi wa mkutano wa Wakuu wa Nchi wanaoshiriki katika mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi (COP 26), unaofanyika hapa Glasgow, Scotland.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea kwenye ukumbi wa Mkutano kwa ajili ya kuhudhuria ufunguzi wa Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP26) unaofanyika Glasgow, Scotland leo tarehe 01 Novemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi Green Climate Fund (GCF) Yannick Glermarec kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26) unaofanyika Glasgow, Scotland leo tarehe 01 Novemba, 2021.

Mara baada ya ufunguzi wa Mkutano huo, Mhe. Rais Samia pia amehutubia moja ya mikutano maalumu uliotishwa na Mawaziri Wakuu wa Uingereza na Italia pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu mapambano dhidi ya Tabianchi COP 26.

Katika mkutano huo uliopewa jina la Action and Solidarity –The Critical Decade Event, Mhe. Rais Samia ameeleza juhudu zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha inakabiliana na majanga ya mabadiliko ya tabianchi ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua madhubuti kwenye sekta za nishati, misitu, usafirishaji na nyinginezo.

Aidha, Mhe. Rais Samia pia ametoa wito kwa nchi zilizoendelea kushikamana na wadau wengine katika kukabiliana na changamoto za tabianchi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi Green Climate Fund (GCF) Yannick Glermarec mara baada ya kuzungumza nae Glasgow, Scotland leo tarehe 01 Novemba, 2021.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Samia amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa kupambana na Mabadiliko ya tabianchi Green Climate Fund (GCF), Bw. Yannick Glermarec na kumshukuru kwa ushirikiano baina ya shirika hilo na Serikali ya Tanzania.

Mhe. Rais Samia amesema kuwa athari za mabadiliko ya tabianchi kwa Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani zimeathiri shughuli za kiuchumi na ujasiriamali kama vile kilimo, utalii na biashara, hivyo fedha zinazopatikana kutoka katika mfuko huo wa zitasaidia Tanzania kuweza kurekebisha athari za mabadiliko ya Tabianchi kwa malengo yanayowezesha kutolewa kwake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera kabla ya kuanza kwa Mkutano wa wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26) unaofanyika Glasgow, Scotland leo tarehe 01 Novemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera kabla ya kuanza kwa Mkutano wa wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26) unaofanyika Glasgow, Scotland leo tarehe 01 Novemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. Boris Johnson (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kulia) mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano mjini Glasgow, Scotland kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano wa COP26 leo tarehe 01 Novemba, 2021.

Vilevile, Mhe. Mhe. Rais Samia ametoa wito kwa mfuko huo wa GCF kutathmini na kuondoa urasimu wa kiutendaji ili nchi zinazopaswa kupokea fedha kutoka mfuko huo kuweza kuzipata kwa muda ili ziweze kufanya kazi iliyokusudiwa.

Kesho tarehe 02 Novemba, 2021, Mhe. Rais Samia anatarajiwa kuhutubia Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanaoshiriki mkutano huo wa COP 26.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news