Rais Samia aipa tiki TANRODAS kwa kazi nzuri

NA MWANDISHI MAALUM

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kutengeneza michoro ya watembea kwa miguu na waendesha baiskeli katika barabara mpya zitakazojengwa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu matumizi ya Barabara alipotembelea mabanda ya maonesho kwenye maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yaliyofanyika Novemba 23,2021 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.Wa pili kulia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro. (PICHA NA IKULU).

Ameyasema hayo Novemba 23, 2021 wakati akizungumza katika Banda ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi katika Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Kitaifa jijini Arusha.

Rais amesema, ujenzi mpya wa barabara unapaswa kuwa na mfumo huo ili kuepusha ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikipoteza uhai wa Watanzania wengi.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Samia ameipongeza TANROADS, kwa hatua ya kuongeza mfumo wa alama kwa wenye ulemavu ambao ni wenye ulemavu wa macho, walemavu wa viungo na albino.

Mtendaji Mkuu wa TANRODS, Mhandisi Rogatus Mativila akitoa taarifa kuhusu wakala huo amesema, TANRODS imekuwa ikitoa elimu ya mara kwa mara kwa watumiaji wa barabara ili kuhakikisha hali ya usalama wa barabara inakuwa bora nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news