Rais Samia ampongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa kuendelea kuiletea Zanzibar maendeleo

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kazi kubwa na nzuri ya kuiletea maendeleo Zanzibar kupitia sekta mbalimbali.
Mama Samia ametoa pongezi hizo katika mkutano maalum ulioandaliwa jijini Zanzibar na Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), kwa ajili ya kumpongeza Mwenyekiti huyo kwa juhudi zake za uongozi uliotukuka.

Amesema, katika kipindi cha mwaka mmoja ya uongozi wake, Dkt.Mwinyi ameonyesha Dira kwa kupiga vita rushwa na ufisadi, hivyo akaahidi Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa maslahi ya wananchi wote, huku akibainisha kuwa Tanzania bila rushwa inawezekana.
Amesema, amani na usalama unaoshuhudiwa hivi sasa hapa nchini, ni zao la Serikali anayoiongoza na akatumia fursa hiyo kuwapongeza Wazanzibari kwa kuunga mkono Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) na kueleza kuwa Serikali hiyo imeonyesha matumaini makubwa.

Mama Samia alisema amani inapotoweka Zanzibar athari zake hufika hadi Tanzania Bara, hivyo akatoa wito wa kudumisha misingi ya amani iliopo.

Nae, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi alimpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiunga mkono na kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi alisema kuwa katika uongozi wa Rais Samia Tanzania imepiga hatua kubwa za maendeleo.

Sambamba na hayo alitoa pongezi kwa Watanzania kwa kuendelea kumuombea dua kwani mambo anayofanya Rais Samia ni makubwa sana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya Ngalawa kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Zanzibar kwa niaba ya UWT Mhe. Swahiba Kisasi katika mkutano ulioandaliwa na Jumuiya hiyo kwa ajili ya kumpongeza katika Viwanja vya Maisara Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwapongeza na kuwatunza Wasanii wa kikundi cha Tarab cha Culture cha Zanzibar kupitia Msanii Sabina Hassan, kwenye mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika katika Viwanja vya Maisara Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Maisara Zanzibar kwa ajili ya kushiriki katika mkutano ulioandaliwa UWT.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Maisara Zanzibar kwa ajili ya kushiriki katika mkutano UWT, Novemba 20, 2021. (PICHA NA IKULU).

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuipongeza UWT kwa wazo zuri walilokuja nalo na pia kushirikiana na Jumuiya zote za CCM kufanikisha jambo hilo kwa msingi kuwa ni lao wote.

Mapema uongozi wa UWT ulimpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa juhudi kubwa anazozichukua katika uongozi wake sambamba na kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi hasa uchumi wa Buluu katika uongozi wake kama Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 ilivyoelekeza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news