Rais Samia ateta na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza

NA MWANDISHI MAALUM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Oktoba 31, 2021 amekutana na kuzungumza na Mjumbe Maalumu wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson katika masuala ya biashara kati ya Uingereza na Tanzania, Lord John Walney.
Bw. Walney amekutana na Mhe. Rais Samia kujitambulisha akiwa na jukumu la kuwa kiungo kati ya nchi hizo mbili kuhusu masuala ya biashara, uwekezaji na utalii.

Amesema, kukutana kwake na Mhe. Rais Samia kumempa fursa ya kujua vipaumbele vya Serikali ya Tanzania ambavyo vitamuwezesha kuwashawishi zaidi wafanyabiashara wa Uingereza kuwekeza katika sekta ya bishara na utalii nchini Tanzania.
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan azungumza na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza katika masuala ya Biashara kati ya Tanzania na Uingereza Mhe. Lord Walney, Glasgow, Scotland.

Kwa upande wake Mhe. Rais Samia amemshukuru Bw. Walney kwa uamuzi wake wa kukutana nae na kujitambulisha kwake na kumueleza kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Uingereza katika kuchochea biashara baina ya nchi mbili hizo.

Mhe. Rais Samia amesema Serikali ya Uingereza na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa kibiashara kwa muda mrefu ambapo Uingereza ni moja kati ya nchi zinazoongoza kuwekeza nchini Tanzania, hivyo kupitia mjumbe huyo kutaongeza fursa zaidi za kibiashara katika kukuza ushirikiano wa uchumi na Uingereza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news