Rais Samia awatunuku Kamisheni maafisa wanafunzi 118 wa JWTZ kundi la O2/18

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo Novemba 22, 2021 amewatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 118 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kundi la 02/18 wa Shahada ya Sayansi ya Kijeshi na kundi la 08/18 Jeshi la Anga, katika sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Jeshi (TMA) Monduli mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitunuku Shahada ya Sayansi ya Kijeshi katika masomo ya kiraia kwa Wahitimu 61 wa JWTZ katika Mahafali ya pili ya Chuo cha Uhasibu yaliyofanyika TMA Monduli mkoani Arusha leo tarehe 22 Novemba, 2021.

Akitoa maelezo ya sherehe hizo, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) Brig. Jen. Jackson Mwaseba amesema kati ya Maafisa hao wanafunzi waliohitimu 62 ni wa shahada ya Sayansi ya Kijeshi inayotolewa na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kwa kushirikiana na Chuo cha TMA na 56 ni wahitimu wa mafunzo ya Urubani.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo amemshukuru Mhe. Rais Samia na Serikali kwa jitihada anazozifanya kuliwezesha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kutekeleza kwa ukamilifu majukumu yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi kundi la 02/18 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika sherehe zilizofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (Tanzania Millitary Academy – TMA) mkoani Arusha leo tarehe 22 Novemba 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimvalisha bawa 2lt. Ibrahim Joseph Mwamboli kuashiria kuhitimu kozi ya Urubani kati ya Maafisa wapya wanafunzi 56 wa JWTZ katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) mkoani Arusha leo tarehe 22 Novemba, 2021.

Aidha, Jen. Mabeyo amewapongeza Maafisa hao wapya kwa kuhitimu mafunzo yao kwa viwango vinavyokubalika na kuwakumbusha kuheshimu, kuthamini, kuzingatia na kutunza kiapo cha Utii walichoapa mbele ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu.

Jen. Mabeyo amewataka Maafisa hao wapya kuwafundisha wafuasi wao maadili mema na kuwa macho na matishio ya ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na Majenerali, Maafisa, Askari na Wageni waalikwa Mhe. Rais Samia amekipongeza Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) na Chuo cha Uhasibu Arusha kwa ubunifu walionyesha katika kutoa mafunzo hayo kwa Maafisa hao wapya wa JWTZ.

Aidha, Mhe. Rais Samia amewapongeza pia Wahitimu wote wa mafunzo hayo ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi kwa kufuzu mafunzo yao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimvalisha bawa Slt. Asnat Rashid Akbar kuashiria kuhitimu katika kozi ya Urubani kati ya Maafisa wapya wanafunzi 56 wa JWTZ katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (Tanzania Military Academy-TMA) mkoani Arusha leo tarehe 22 Novemba, 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wapya wa JWTZ katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli TMA mkoani Arusha leo tarehe 22 Novemba 2021 baada ya kuwatunuku Nishani Maafisa hao. Maafisa wapya wa JWTZ katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli mkoani Arusha leo tarehe 22 Novemba 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifunga mafunzo kwa wahitimu wapya katika ngazi ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi katika masomo ya kiraia kwa Wahitimu 61 wa JWTZ katika Mahafali ya pili ya Chuo cha Uhasibu yaliyofanyika Monduli mkoani Arusha leo tarehe 22 Novemba 2021. Maafisa wapya wa JWTZ wahitimu katika ngazi ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi katika masomo ya kiraia ya Mahafali ya pili ya Chuo cha Uhasibu Monduli Arusha leo tarehe 22 Novemba 2021. 

Pamoja na kutunuku Kamisheni, Mhe. Rais Samia ametoa zawadi kwa Maafisa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi na kuwavisha mabawa Maafisa wapya wawili kwa niaba ya wenzao ikiwa ni ishara ya kuhitimu mafunzo yao ya urubani.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amempongeza Mhe. Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwa ni pamoja na kukiwezesha Chuo cha Uhasibu Arusha kutoa mafunzo ya Shahada ya Usalama wa Kimtandao (Cyber Security).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mkuu wa Itifaki wa JWTZ Kanali Kobero wakati wa Mahafali ya pili ya Chuo cha Uhasibu yaliyofanyika TMA Monduli mkoani Arusha leo tarehe 22 Novemba, 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wapya katika ngazi ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi katika masomo ya kiraia katika Mahafali ya pili ya Chuo cha Uhasibu Monduli Arusha leo tarehe 22 Novemba 2021. (PICHA ZOTE NA IKULU).

Sherehe za kuwatunuku Kamisheni Maafisa hao zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax, Waziri wa Fedha pamoja na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba. Wengine ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi kutoka mikoa mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news