RC Mahenge awashukuru viongozi wa dini kwa kuunga mkono mapambano dhidi ya UVIKO-19

NA MWANDISHI MAALUM

MKUU wa Mkoa wa Singida,Dkt.Bilinith Mahenge ameyapongeza na kuyashukru madhehebu mbalimbali ya dini,kwa maamuzi yao ya kuunga mkono juhudi za serikali za mapambano dhidi ya Virusi Vya Korona ambavyo vinasababisha homa kali ya mapafu (UVIKO-19).
Dkt.Mahenge ametoa pongezi hizo wakati akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa mkutano uliohudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki nchini mkoani hapa.

Mkutano huo wa siku tatu, unaendelea kwenye ukumbi wa mikutano Jimbo la Singida na unahusu uhamasishaji wa chanjo ya UVIKO-19 kwa Watanzania.

Amesema, mapambano dhidi ya gonjwa hatari la UVIKO-19,sio ya serikali peke yake ni la Watanzania wote wakiwemo wa madhehebu ya dini washiriki.

Amefafanua kwamba, mafanikio yatakayopatikana kwenye kikao au mkutano huo yatasaidia viongozi wa serikali na madhehebu ya dini,kuongea lugha moja katika kulinda afya za waumini na jamii kwa ujumla dhidi ya UVIKO-19.

“Kikao hiki pia kitatuongezea kanuni na mbinu za kusaidia kuzungumza na waumini kuhusu athari za ugonjwa wa Korona.Muhimu zaidi ni kuwakumbusha waumini mara kwa mara kuhusu umuhimu wa kupata chanjo ya UVIKO-19,”,amesema.

Aidha,Dkt.Mahenge amesema, Wizara ya Afya inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na taasisi za dini mbalimbali hapa nchini.

“Kanisa Katoliki kupitia taasisi zake na maelekezo ya viongozi wa ibada,mlishiriki kwa nafasi zenu mlisaidia sana kupunguza hofu katika jamii yetu.Kipekee zaidi mlishirikiana na serikali katika kuhakikisha jamii yetu inajikinga na ugonjwa huu ambao umesababisha vifo vya watu wengi duniani,”amesema mkuu huyo wa mkoa.

Kwa upande wa mkoa wa Singida,amesema mkoa hadi juzi umechanja watu 26,739 kati ya watu 1,754,370 wamekwisha maliza dozi ile ya Jensen sawa na asilimia 1.5.

“Kwa sasa nchi imepokea chanjo ya aina ya Sinopharm na zoezi la uchanjaji linaendelea nchi nzima.Chanjo ya Sinopharm wataalamu wanasema ni dozi mbili,hivyo elimu na mikakati zaidi,inahitajika.Chanjo hii ni kwa ajili ya mchajaji kujilinda na watu wengine pia,”amesema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma wa Wizara ya Afya,Dkt.Ama Kisangala amesema, lengo la mkutano huo ni kuwajengea viongozi uwezo zaidi ili wakawe mabalozi wazuri katika kuelimisha jamii kuhusu madhara ya korona.

Wakati huo huo,Padri kanisa Katoliki Mkoa wa Tabora,Padri Dkt.Chobo Steve Paul ameongeza kwamba, lengo la mafunzo hayo ni kufikisha elimu hiyo katika majimbo yote nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news