Serikali yapongeza ujenzi Kituo cha Afya Mtama kwa kuzingatia ubora

NA FRED KIBANO

SERIKALI imeridhishwa na ujenzi wa kituo cha afya Mtama katika Halmshauri ya Wilaya ya Mtama mkoani Lindi na kwamba waendelee kuzingatia ubora wanaotumika katika ujenzi wao.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange (MB) ametoa pongezi hizo alipofanya ziara yake wilayani humo kwa kuangalia ujenzi wa kituo ambao thamani ya fedha inaonekana na unakwenda kwa kasi inayotakiwa.

Pia amebaini wanazingatia ubora unaotakiwa na hivyo amewaasa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo na watendaji wake kuendelea kusimamia ubora hasa katika hatua za umaliziaji ili majengo yasipoteze thamani yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtama, Bw. George Mbilinyi amesema wanatarajia kukamilisha majengo yote matatu kwa wakati na kwamba endapo watapatiwa fedha za awamu ya pili kituo hicho kitapiga hatua kubwa ya miundombinu kuelekea kutoa huduma za afya kwa wananchi wa Mtama.
Awali akisoma taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtama, Dkt. Dismas Masulubu amesema, ujenzi wa kituo cha afya tarafa ya Mtama unajengwa kutokana na fedha za tozo ambapo kituo hicho kilipokea shilingi milioni 250 na kwamba fedha hizo zinatumika kujenga majengo matatu ya wagonjwa wa nje ambalo limefikia asilimia 45, maabara asilimia 50 na kichomea taka ambacho bado hakijajengwa. Aidha, wanajeshi wamejitolea nguvu zao kwa kusafisha eneo na kazi nyingine nyingi za mikono.

Amesema, kiasi cha fedha kilichotumika mpaka sasa ni shilingi 112,172,991 na salio shilingi 137,827,009 fedha zinazofanya kazi ya umaliziaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news