Shaka aanza kuzisaka kura 11,500 kwa ajili ya Emmanuel Shangai jimboni Ngorogoro

NA MARY MARGWE

KATIBU wa NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi, Mlezi wa Mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Shaka Hamdu Shaka ameanza rasmi kuzisaka kura 11,500 kwa ajili ya mgombea Ubunge Jimbo la Ngorogoro, Emmanuel Shangai.
Ni katika uzinduzi wa kampeni ambapo Shaka aliongozana na viongozi mbalimbali wa chama kutoka Makao Makuu ya CCM Taifa wakiongozwa na Katibu wa Nec, Idara ya Organaizeshen Dkt. Maudline Castico Uwanja wa Malambo, Kata ya Malambo, Tarafa ya Sale.
Katibu wa NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi, Mlezi wa Mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Ndg. Shaka Hamdu Shaka akimnadi mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM ), Emmanuel Shangai, baada ya uzinduzi wa kampeni Novemba 26,2021.
Kura hizo zinatokana na wapiga kura 11,500 katika Jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha ambao wanatarajia kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo hilo unaotarajiwa kufanyika Desemba 11,2021.
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro,Dkt.Jumaa Mhina amesema wapiga kura hao ni kwa mujibu wa kumbukumbu za daftari la mpiga kura la mwaka 2020.
Uchaguzi huo mdogo unafanyika kufuatia aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, William Ole Nasha kufariki dunia,Septemba 27 mwaka huu mjini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments