TFS yashiriki Kongamano la Utalii mjini Kigali

NA MWANDISHI MAALUM

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) inashiriki katika Kongamano la 4 la Uongozi wa Utalii Afrika (ATFL- Africa Tourism Leadership Forum) linalofanyika kwa mara ya kwanza nchini Rwanda likiambatana na wiki ya maonesho ya Utalii kwa mwaka 2021 inayofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Kigali.
Afisa Mhifadhi TFS, Yusuph Tango (Kushoto) akita maelezo kwa wageni waliofika kujua kuhusu utalii ikolojia mapema jana katika Hoteli ya Serena Kigali Rwanda. (Picha na TFS).

Yusuph Tango ni Afisa Mhifadhi TFS, anasema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelenga kulitumia kongamano hilo na wiki ya Maonesho ya utalii katika kutangaza vivutio vyetu vya utalii, bidhaa na huduma mbalimbali tunazozitoa katika sekta ya utalii na mikakati kurejesha na ukomavu wa sekta ya utalii baada ya mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO -19

“Lengo kubwa la Kongamano hili ni kuona jinsi nchi mbalimbali na wadau wa sekta ya utalii walivyojipanga na wanavyoendelea kuweka mikakati ya kurejesha biashara katika sekta ya utalii baada ya janga la UVIKO-19 ili kuwa na uchumi jumuishi na maendeleo endelevu ya sekta ya utalii barani Afrika lakini pia kuangalia jinsi nchi za Afrika zinavyoweza kuuza vivutio vyake kwa nchi zilizoendelea,"amesema.“Sisi TFS tumetumia fursa ya maonesho haya kutoa elimu ya uhifadhi kwa kuonyesha umuhimu wa kuhifadhi Misitu ambayo ni makazi ya Wanyamapori, lakini pia vyanzo vya Maji ya mito, lakini pia tunawaeleza fursa za kuja kujionea na kufurahia utalii ikolojia katika misitu yetu iliyohifadhiwa, vituo vyetu vya malikale na hata kuja kuwekeza kwa kuanzisha miradi katika sekta ya utalii na hasa maeneo ya Utalii ikolojia,”ameongeza Tango alipohojiwa na Mwandishi wetu leo.

Katika Kongamano hilo la 4 la Uongozi wa Utalii Afrika linalofanyika kwa mara ya kwanza nchini Rwanda, washiriki kutoka Taasisi za serikali, mashirika ya umma na sekta binafasi zilizopo katika sekta ya utalii, ukarimu, hoteli na mnyororo mzima wa sekta ya utalii barani Afrika kutoka ndani na nje ya nchi wameshiriki

Maonesho haya yametoa fursa kwa wadau mbalimbali katika sekta ya utalii na sekta nyingine wezeshi kukutana, kufahamiana na kubadilishana uzoefu katika uendeshaji na ukuzaji wa sekta ya utalii baada ya nchi nyingi kukumbwa na changamoto ya kuendesha shughuli za Utalii baada ya janga la UVIKO-19.

Kongamano hilo na wiki ya Maonesho ya utalii limeanza Novemba 24 hadi 27, 2021 na kuhudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania.

Dhima ya maonesho hayo kwa mwaka huu ni 'Harnessing intra-Africa travel for innovative recovery in Africa's travel and tourism sector'.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news