Uswisi yaridhishwa na kasi ya maendeleo Tanzania

NA MWANDISHI DIRAMAIKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uswisi Bi. Patricia Danzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uswisi ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bi. Patricia Danzi, wakati ujumbe huo ulipofika Jijini Dodoma. (PICHA NA IKULU).

Katika Mazungumzo hayo ya Novemba 26, 2021 jijini Dodoma, Bi. Danzi amempongeza Mhe. Rais Samia kwa maendeleo makubwa yaliyopatikana nchini Tanzania kwa kipindi kifupi tangu aingie madarakani ikiwa ni pamoja na Serikali kuruhusu watoto wa kike waliopata ujauzito kurudi shuleni.

Bi. Danzi amemueleza Mhe. Rais Samia kuwa Serikali ya Uswisi imekuwa na ushirikiano wa kimaendeleo na Serikali ya Tanzania kwa zaidi ya miaka 40 katika sekta za afya, elimu katika masuala ya utafiti na kuwawezesha vijana katika mipango mbalimbali ya maendeleo.

Kwa upande wake Mhe. Rais Samia ameishukuru Serikali ya Uswisi kwa ushirikiano na uhusiano wa muda mrefu katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.

Mhe. Rais Samia pia amemueleza Bi. Danzi hatua zinazo chukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kuimarisha huduma za jamii kwa wananchi ikiwa ni pamoja na sekta ya elimu, maji, afya na nyinginezo.

Kuhusu UVIKO 19, Mhe. Rais Samia amemueleza Bi. Danzi kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali za kukabilaiana na ugonjwa huo ikiwemo kutoa chanjo na elimu kwa wananchi katika ngazi mbalimbali. Tayari Mhe. Rais Samia amewasili jijini Dar es Salaam akitokea jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam akitokea mkoani Dodoma. (PICHA NA IKULU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news